Mbowe alivyotoka kuwahutubia wafuasi wake nyumbani

Dar es Salaam. Wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamekusanyika nyumbani kwa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, Mikocheni jijini Dar es Salaam kwa lengo la kumshawishi achukue fomu kuwania tena nafasi hiyo.

Wafuasi hao wakiwa na shangwe na hamasa, wamefanya hivyo kama ishara ya kumuunga mkono, wakimsihi aendelee kuongoza chama hicho.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amerejesha fomu ya kuwania nafasi ya uenyekiti wa chama na kupokelewa na Naibu Katibu Katibu Mkuu- Bara, Benson Kigaila.

Lissu amerejesha fomu hiyo leo Jumatano, Desemba 18, 2024 katika ofisi za Makao Makuu ya Chadema, Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Wakati Lissu akirejesha fomu hiyo, makada wa wafuasi wa chama hicho muda huu wako nyumbani kwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

Wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakiwa nyumbani kwa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe Mikocheni jijini Dar es Salaam. Picha na Sunday George

Makada hao wamefika nyumbani kwa Mbowe, Mikocheni jijini Dar es Salaam, kumshawishi achukue fomu kutetea nafasi hiyo. Muda wowote kutoka sasa Mbowe atakuwa anazungumza na makada hao waliofika nyumbani kwake tangu asubuhi.

Related Posts