Gymkhana kumekucha na Lina PG Tour

RAUNDI ya tano ya Linar PG Tour inatarajiwa kuanza kesho kwenye viwanja vya Dar Gymkhana, kuhitimisha michuano ya gofu ya mwaka huu, huku mshindi akiondoka na Sh8.8 milioni.

Mbali na zawadi hiyo fedha hizo, mshindi wa jumla pia atakata tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa jijini Dubai, Failme za Kiarabu mwakani.

Kama ilivyokuwa raundi nne za awali, mshindi wa gofu ya kulipwa ataondokana na Sh6.8 milioni, wa gofu ya ridhaa atajipatia Sh2 milioni, huku washindi wengine tisa wanaofuata wakinufaika na zawadi hizo.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa mashindano hayo, Yasmin Challi michuano hiyo itapigwa siku nne kwa mashimo 18 kwa siku na kukamilisha mashimo 72 itakapokamilika na inashirikisha wanaume na wanawake.

Alisema leo Alhamisi na kesho Ijumaa zitachezwa raundi mbili za mchujo ili kuwapata wachezaji bora watakaocheza fainali katika mashimo 36 ya mwisho.

Mchuano mkali unatarajiwa kuwa kwa washiriki Nuru Mollel anayeongoza mbio za ubingwa baada ya kushinda raundi tatu kati ya tano, akifuatiwa na Fadhil Nkya na Isack Wanyeche, huku kwa upande wa gofu ya ridhaa, mchuano mkali utakuwa kwa Ally Isanzu na Isiaka Daudi Mtubwi.

Related Posts