Ngo’s zatakiwa kufanya kazi Kwa kuzingatia maadili.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mashirika yasiyo ya kiserikali Taifa Bi. Mwantumu Mahiza amezitaka taasisi zisizo za Kiserikali (NGOs) Mkoani Morogoro kufanya kazi zao kwa uwazi, ukweli na kujituma zaidi kwa kujua kuwa wanafanya kazi pamoja na serikali katika maeneo yao na kwa kushirikiana na madiwani, wenyeviti wa vitongoji na vijiji.

Mahiza ameyasema hayo Mkoani Morogoro wakati wa kikao na taasisi hizo Ili kuwajengea uwezo namna ya Kufanya kazi vizuri kwa kufuata maadali ,sera na utamaduni wa Kitazania.

Amesema baadhi ya mashirika yamekuwa yakifanya kazi kinyume na taratibu na Sheria za nchi jambo ambalo ni kinyume na utaratibu za utendaji kazi ka mashirika hayo.

Kwa Upande wake Mkuu Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima ametaka uwepo ushirikiano wa kutosha baina ya mashirika yasiyo ya kiserikali na serikali kwa kuwa na misingi ya kuaminiana kwa kila pande ili kulinda maslahi ya Mkoa na Taifa kwa ujumla.

Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa amesema mashirika hayo yana uhuru wa kufanya kazi lakini yanapaswa kushirikiana na serikali ili kuendelea kuondoa kasoro ndogo ndogo zilizopo na kuyataka kufuata taratibu, kanuni na sheria za kujisajili na namna ya kuendesha kazi zao kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla.

Naye, Mwakilishi wa Mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoa wa Morogoro Bw. Otanamus Nicholas ameyashukuru mashirika hayo kushiriki kikao hicho  ambapo amesema kimeweka wazi utekelezaji wa kila shirika na kunuia kufanya kazi na Serikari inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kuwaletea tija wananchi wake.

   

 

Related Posts