Na Chalila Kibuda ,Michuzi Tv
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limesema kuwa linaendelea na ukaguzi vyombo vya usafirishaji majini kutokana na baadhi vyombo vyombo hivyo kuzidisha abiria au mizigo katika Siku kuu za mwisho wa mwaka.
Akizungumza katika ukaguzi wa Meli ya Zan Fast Farries Afisa Mkaguzi Mkuu wa Shirika hilo Rashid Katonga uliofanyika Bandarini jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa TASAC katika kuhakikisha abiria wanasafiri kwa usalama wao unahitajika katika kufanya ukaguzi kwa vyombo vya usafirishaji majini.
Hata hivyo amesema katika ukaguizi huo walianza na ukaguzi wa meli za Azam za Kilimanjaro na kufuatia Meli za Zan Fast Farries ambapo vyombo hivyo vinafuata sheria.
Katonga amesema kuwa katikq kipindi hiki kumekuwa na baadhi ya vyombo vya usafirishaji majini kuongeza idadi ya abiria au mizigo kutokana na kuwepo kwa uhitaji wa watu wengi kufanya safari au kusafirisha mizigo.
Amesema katika kipindi hiki TASAC imejipanga kufanya ukaguzi kwa kuangalia uwezo wa chombo na abiria wanaotakiwa na wakibaini safari inasitishwa pamoja kulipa gharama za ukiukaji wa sheria.
Aidha Amesema kuwa ukaguzi huo unakwenda pamoja na kutoa elimu kwa abiria katika kuwakumbusha wajibu wa kusafiri kwa kutumia vyombo hivyo.
Manahodha wa Zan Fast Farries wamesema kuwa ukaguzi huo unawasaidia wao kwani wamiliki wanaweza kutaka chombo kiondoke licha ya kuwa na changamoto lakini changamoto hizo kwa mamlaka ya TASAC wanazuia.
Aidha amesema kuwa licha ya kufanyiwa ukaguzi Zan Fast Farries tuna utaratibu kufanya ukaguzi wa mara kwa mara.
Hata hivyo manahodha hao wamesema TASAC wanawasaidia sana katika kuwalinda manahodha katika maeneo mbalimbali.
Manahodha wamesema. kuwa TASAC kufanya ukaguzi ni jambo zuri kutokana kukumbusha wasafirishaji kuelewa wajibu katika vipindi vyote katika kulinda maisha ya wasafiri.
Wameongeza kuwa wataendelea kutoa huduma kwa kufuata sheria zilizowekwa mamlaka pamoja kufanya ukaguzi wao binafsi wa vyombo hivyo.
Mwenyekiti wa Umoja Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Ali Kawaida amesema kuwa amesafiri salama na Zan Fast Farries na kuongeza kuwa ukaguzi ni mzuri katika kuhakikisha wananchi wanakuwa salama.
Amesema TASAC kwa utaratibu wa ukaguzi vyombo vya usafiri majini waendelee ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wasafiri juu ya usalama wao.
Afisa Mkaguzi Mkuu wa TASAC Rashid Katonga akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ukaguzi wa Meli ya Zan Fast Farries jijini Dar es Salaam.
Abiria wakikaguliwa tiketi kwa ajili ya safari kwenda Zanzibar.