Viongozi wa dini Mkoa wa Kagera wafanya maombi maalum

Renatha Kipaka, Bukoba

Viongozi wa Mkoa wa Kagera kwa kushirikiana na viongozi wa dini umefanya maombi maalum ya kuliombea Taifa ili liendelee kuwa na amani, mshikamano, utulivu pamoja na maendeleo.

Maombezi hayo yamefanyika mjini Bukoba kwa kushilikisha wananchi na waumini wa madhehebu mbalimbali.

Hata hivyo Padre Samueli Muchunguzi, Makamu Askofu wa Kanisa Katoliki la Bukoba, amesisitiza umuhimu wa kumtegemea Mungu katika kila jambo. Akirejea Zaburi 127:1, amesema: “Bwana asipojenga nyumba, wajengaji wanafanya kazi bure; na asipolinda mji, walinzi wanakesha bure.”

Padre Muchunguzi amewaombea wananchi kuishi kwa uadilifu, kutenda haki, na kuachana na chuki na wivu. Amesema tabia hizi zimekuwa kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya mkoa wa Kagera.

Kwa upande wake, Sheikh wa Mkoa wa Kagera, Haruna Kichwabuta, amewaombea wananchi na viongozi kuishi kwa upendo, uvumilivu na amani ili kujenga taifa lenye ustawi na linalovutia ndani na nje .

Shughuli hiyo pia ilihusisha maombi ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, viongozi wake, na wananchi kwa ujumla.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Hajat Fatma Mwassa, amesema dua na maombezi hayo ni sehemu ya maandalizi ya Tamasha la Ijuka Omuka 2024, ambalo linaangazia fursa mbalimbali zinazopatikana mkoani Kagera.

Amefafanua kuwa tamasha hilo limeanzishwa kwa lengo la kuwakutanisha wazawa wa Kagera na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi ili kushirikiana katika kuendeleza mkoa huo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajjat Fatma Mwassa amesema kuwa tukio hilo lilikuwa nisehemu ya kufungua tamasha la Ijuka Omuka 2024 lenye lengo la kuhamashisha furusa mbalimba za maendeleo.

Related Posts