Waitara ahoji bungeni mwarobaini mauaji katika mgodi Barick North Mara

MBUNGE wa Tarime Vijijini (CCM), Mwita Waitara, ameitaka Serikali kutafuta mwarobaini wa visa vya mauaji ya vijana wanaodaiwa kuvamia maeneo ya Mgodi wa Barrick North Mara, baada ya kukosa maeneo rasmi ya kutekeleza shughuli zao za uchimbaji. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza bungeni jijini Dodoma, leo Ijumaa, Waitara amedai kuna mgogoro kati ya mwekezaji huyo na vijana wazawa, ambao unaleta madhara ikiwemo majeruhi na hata mauaji.

Mwita Waitara

“Mgodi wa Barrick North Mara Nyamongo kumekuwa na matatizo ya madhara ya hapa na pale majeraha na mauaji kwa sababu vijana wanahitaji maeneo ya wachimbaji wa dogo. Ningetamani kujua ili kutenganisha mgogoro ulioko pale ni lini Serikali itachukua maeneo ambayo mgodi hauwezi kuchimba kuwakabidhi wananchi ili kupunguza malalamiko?” amesema Waitara.

Naibu Waziri wa Madini, Dk. Steven Kiruswa, amesema wizara hiyo imemuomba mwekezaji awasaidie wachimbaji wadogo kufanya utafiti katika maeneo yanayozunguka mgodi wake na kutoa maeneo ambayo inaona haitumii kwa ajili ya uzalishaji ili wapewe vijana waache kuvamia kila wakati na kusababisha madhara.

Related Posts