TRA WAWASHUKURU WALIPAKODI WA KATI KISEKTA

Kaimu Naibu kamishna walipa kodi wa Kati kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Godwin Barongo akiwaaga wafanyakazi wa SAS Logistics Ltd  mara baada ya kuwatembelea katika ofisi zao zilizopo Tabata wakati Mamlaka ya Mapato Tanzania walipowatembelea mahali pa kazi jijini Dar es Salaam leo Desemba 19, 2024 kwaajili ya kuwashukuru kuwa walipakodi wazuri.

Kulia ni Meneja Mkuu wa SAS Logistic LTD, Adam Ambar akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya mapato Tanzania wakiongozwa na Kaimu Naibu kamishna walipa kodi wa Kati kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Godwin Barongo leo Desemba 19, 2024 walippowatembelea kwaajili ya kuwashukuru kwa kuwa walipakodi wazuri.

MAMLAKA ya Mapato Tanzania kupitia Idara ya Walipakodi wa Kati leo wamewatembelea na kuwashukuru kampuni ya Usafirshaji wa Mizigo ya SAS Logistic Ltd  iliyopo Tabata pamoja na Kampuni ya Uuzaji wa Magari ya FAW iliyopo Tazara jijini Dar es Salaam.

Kaimu Naibu kamishna walipa kodi wa Kati kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Godwin Barongo akizngumza leo Desemba 19, 2024 wakati wa ziara hiyo amewashukuru ya walipakodi hao kwa kuwa walipakodi wazuri katika kipindi kilichopitta. 

Pia  amewaomba kuwa na ushirikiano na Mamlaka hiyo katika kipindi kipya Cha miezi sita kinachokuja.

“Tunaamini mchango wao ni muhimu kwetu wote na ni muhimu kwa Taifa na ni muhimu kwa Watanzania wote kwa ujumla.” Amesema Barongo 

 “Tumekuja hapa kwa mteja wetu, tukiwa kwenye mfululizo wa kuwashukuru walipa Kodi  wetu ambao tumekuwa nao kwa kipindi Cha miezi sita wamekua na mchango mkubwa kwetu na wamekuwa na mchango mkubwa kwa taifa hivyo tumeona ni vyema kuja wakushukuru kwa mchango huo lakini pia kuwatakia heri ya krismasi na mwaka mpya.

Aidha Barongo ametoa wito kwa watanzania wote kwa ujumla kulipa Kodi kwahiari na kwa wakati,  kwa wale ambao wanatakiwa kulipa kodi ya ongezeko la thamani VAT amewaomba kukamilisha kulipa kwani siku ya mwisho ni kesho  tarehe 20, Desemba 2024 hivyo wahakikishe wanakwenda kulipa Kodi zao.

Kwa Upande wa Meneja Mkuu wa SAS Logistic LTD, Adam Ambar amewashukuru TRA kwa kuwatambua katika kama ni walipaji wa wazuri kwani kodi ni kwaajili ya kuchochea Maendelea ya kila mmoja pamoja na taifa kwa ujumla.

“Sisi kama SAS Logistics tunashukuru kwani mmetukumbuka mmeona, msingekuja bila kuona… Na sisi tunashukuru kwa kututambua na tutaendelea kuiunga mkono serikali ya  Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na sisi tumejiwekea kwamba hakuna kodi itakayopotea tukiwa sisi tupo hapa kwasababu chakwako chukua cha wenzako wape hiyo kwetu ndio kanuni yetu.” Amesema Ambar 

Akizungumzia changamoto wanazozipata kama kampuni ya usafirishaji, Ambar  amesema kuwa kunachangoto katika mizani ya Mikumi ‘Check Point’ ya uelewa wa watumishi

Akizungumza wakati walipotembelewa ofisini kwao wanapouza Magari, Afisa Mwajili wa FAW, Happy Mjema amewashukuru ugeni wa TRA…

 “Tunawashukuru ugeni wa TRA ulioambatana na Naibu Namishna wa TRA nakutupongeza kwa jinsi tunavyoshirikiana nao vizuri na pia kututakia heri ya krismasi na mwaka mpya katika mwaka tunaolekea wa 2025 tunashukuru sana tunawapenda na karibuni tena.” Amesema Happy

Related Posts