Mradi wa ujenzi wa barabara ya bandari yenye urefu wa kilomita 2.1 wazinduliwa

Kingozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Godfrey Eliakimu Mnzava amezindua Mradi wa ujenzi wa barabara ya bandari yenye urefu wa kilomita 2.1 iliogharimu zaidi ya shilingi milioni 14.89 iliopo katika Kata ya kurasini Wilayani Temeke Jijini Dar es salaam .

Mnzava amesema kukamilika kwa barabara hio itasaidia kupunguza changamoto ya msongamano wa magari bandarini hivyo barabaran hio ndio lango kuu la uchumi wa Temeke.

Wakati huo huo mewatoa shaka wakazi wa Temeke Kwa kuwahakikishia kuwa barabara hio itawanufaisha Wananchiwaliopo Wilayani humo.

Nae Mbunge wa Jimbo la Temeke Dorothy Kilave akizunguza Kwa niaba ya Wananchi wa Temeke amesema kukamilika Kwa barabara hio ni faraha kubwa hivyo amemuomba Kiongozibwa Mbio za Mwenge aweze kuwafikishia Salam zao Kwa Rais Dr Samia Suluhu Hassan kuwa watahakikisha uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi Mkuu watapiga kura na kuwachagua Viongozi sahihi.

Related Posts