Kampuni ya ubashiri Tanzania Meridianbet katika suala zima la kuendeleza sekta ya michezo na imeungana na Timu ya Jogoo Veteran iliyopo Mbezi Juu na kutoa jezi mpya kwa wachezaji wa timu hiyo, ili kuunga mkono juhudi za kukuza michezo katika jamii.
Timu ya Jogoo Veteran, ambayo inajivunia wachezaji wao wenye uwezo na kujituma kwelikweli, inajulikana kwa kuhamasisha vijana na jamii kwa ujumla kuhusu umuhimu wa michezo katika afya na maendeleo ya kijamii. Kwa msaada huu wa jezi kutoka Meridianbet, timu hiyo inatarajia kuendelea kufanya vizuri katika mashindano yao na kuongeza ari ya michezo miongoni mwa wakazi wa Mbezi Juu.
Jumamosi ya leo una nafasi ya kuwa bingwa na Meridianbet kwani odds kubwa na machaguo zaidi ya 1000 yapo hapa. Pia cheza michezo ya Kasino ya mtandaoni kama vile, Poker, Super Heli, Roullette, Aviator, Wild Icy Fruits, Keno na mingine kibao.
Kwanza kabisa timu nzima za Meridianbet ilikaribishwa na Diwani wa Mbezi Juu Mheshimiwa Anna Lukindo, ambaye alifurahi sana kuona ujio huo wa Meridianbet kwani wanasapoti wanamichezo.
Akizungumza wakati wa ugawaji wa jezi hizo, kukabidhi, Mhariri wa Meridianbet, Bi Nancy Ingram, alisema: “Tunajivunia sana kutoa msaada huu kwa Timu ya Jogoo Veteran, ambayo imekuwa nguzo muhimu katika kukuza michezo na umoja wa jamii hii. Tunategemea kwamba msaada wetu utaongeza nguvu kwa timu na kuhamasisha vijana wengi zaidi kushiriki katika michezo.”
Kwa upande wao, viongozi wa Timu ya Jogoo Veteran walishukuru Meridianbet kwa msaada wao, wakisema kwamba jezi mpya zitakuwa chachu ya kuongeza morali kwa wachezaji na kuhamasisha vipaji vipya miongoni mwa vijana.
Pia waliendelea kusema kuwa, “Huu ni msaada mkubwa kwetu, na tutahakikisha kwamba tunafanya mazoezi zaidi na kupambana kwa nguvu ili kuleta matokeo bora.”
Ikumbukwe kuwa hii ni moja ya juhudi za Meridianbet katika kuunga mkono maendeleo ya michezo na kukuza afya njema kwa jamii mbalimbali nchini Tanzania. Kampuni hiyo inaendelea kushirikiana na timu mbalimbali za michezo ili kuhakikisha kuwa michezo inakuwa sehemu ya maisha ya kila mtu.