Shahidi wa Maji wawafikiwa Watu Milion 2.5 elimu ya utunzaji vyanzo vya maji

Zaidi ya Watu milioni Mbili(2.5) nchini wamefikiwa na elimu ya uhifadhi na Utunzaji wa rasilimali za maji ambayo wamepatiwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Shahidi wa Maji.

Akizungumza katika hafla maalum ya kuwatunuki vyeti baadhi ya Wadau wa maji iliyofanyika Mjini Morogoro Mkurugenzi wa Shirika hilo Abel Dugange amesema kundi hilo limekuwa muhimu hasa vijijini katika kuhakikisha Wananchi wanapata huduma ya maji.

Dugange amesema kwenye maeneo ya wafugaji na wakulima Wadau hao wamefanikisha kutatua changamoto migogoro ya wakulima na wafugaji hasa Wilaya Kilosa kwenye vijiji vya Chanzuru na Mbwade Kwa kuweka usawa katika matumizi ya maji.

Amesema Wadau hao wamefanya Kazi ya kushirikiana na Shirika la.Shahidi wa Maji Kwenye bonde la Mto Msimbazi na Mkoani Dar es Salam na Ngerengere Mkoani Morogoro.

Aidha amesema Wadau wamekuwa wakipaza sauti kwa Serikali na Wadau katika masuala yote yanayohusu huduma ya maji,Utunzaji vyanzo vya maji,

Kwa upaande wake Mkuu Wilaya ya Morogoro Mussa Kilakala amesema suala la usimamizi wa vyanzo vya maji ni jukumu la Kila Mtu sio la Serikali pekee.

Kilakala amesema Mkoa wa Morogoro unategemeaa Kwa zaidi ya asilimia 70 upatikanaji wa maji Kwenye mikoa ya Dar es salama na Pwani hivyo lazima jamii iwajibike katika Utunzaji wa vyanzo vya maji

Kwa Upande wake kaimu Mkurugenzi Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu amesema Licha ya changamoto mbalimbali lakini bado wanaendelea kutoa elimu kwa Watu wanaishi jiriani na vyanzo vya maji kuvitunza .

Amesema endapo vyanzo hivyo visipotunzwa ipasavyo hata fedha mbalimbali za ujenzi wa miradi ya Maji hazitakuwa na umuhimu

Shirika la Shahidi wa Maji kwa kushirikiana na mdau wake Water Witness international ya nchini Uingereza wanatekelezea awamu ya tatu ya Program ya uhakiki wa Maji nchini.

Programu hii inalenga kuboresha usimamizi wa Rasilimali za Maji na upatikanaji wa huduma ya Maji kwa Jamii,program inayofadhiliwa na Shirika la Hewllett Foundation lililopo Nchi Marekani ambapo utekelezaji wake umeanza mwezi machi mwaka 2022 hadi Disemba 2024.

  

 

Related Posts