UMOJA wa Wafanyabiashara wa Mahiwa na Nzigua wamemuomba Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuingilia kati operesheni ya kuondoa wafanyabiashara wa kanzu, Mitandio pamoja na vitu mbalimbali vya maharusi wa dini Kiislamu katika barabara ya Mahiwa na nzigua.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Maadili Kasimu Kumbawene wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Desemba 21, 2024, amesema tatizo lilianzia Oktoba 19, 2024 kampuni ya Bakhresa iliomba kibali cha ukarabati wa barabara ya Mahiwa na zigua.
“Kwahiyo tunamuomba sana Mama Samia aweze kusitisha zoezi la Jumatatu kwani litakuja kuleta picha mbaya kwani sisi tunanung’unika kwanini tuondolewe sisi tuu utaratibu na busara vitumike na sisi tutafuata utaratibu utakaopangwa.”
Alikuja Mhe. Awadhi kutuomba tuziondoe meza ili ukarabati ufanyike kwa sababu baada ya ukarabati mtapata manufaa na sisi tukaliona hili mingoni mwa wanufaika wa barabara tutakuwa sisi na sisi hatukuona kipingamizi katika hilo tukashauriana na yeye tukaomba sehemu ya kuhifadhi meza zetu akatuelekeza kuhifadhi mbele ya msikiti ambapo kunachuo, baada ya siku tatu kuanzia Jumatatu, Jumanne kufikia jumatano kukaletewa afisa polisi wa jamii na kutuambia hatutaruhusiwa kurudi katika maeneo haya na kule mbele mtaa wa livingstone na Mahiwa kuliwekwa geti na Mchikichi Nzigua kuliwekwa kuonesha kwamba sisi hatutakiwi kurudi na kukaletwa walinzi kampuni binafsi kuzuia sisi tusifanye biashara.
Amesema jambo la kwanza kwa sababu wanamahusiano mazuri na Msikiti, tukawafuata viongozi wa Msikiti kuwauliza kuhusiana na hilo jambo,…. Viongozi wa Msikiti wakasema wao hawahusiki hili jambo lipo chini ya Bakhresa na huku tetesi zinasema amenunua barabara kwamba hatutakiwa kurudi… Tukaenda kwa Awadhi tena… Tukaongea nae zaidi ya vikao vitatu “ Akasema Bakhresa hataki kuona Uchafu.”… Sisi familia zinatutegemea.” Amesema Kumbawene
Kwa Upande wa Mwenyekiti wa wafanyabiashara Mahiwa na Nzigua, Ramadhani Ally amesema alipewa taarifa na serikali ya mtaa ili aweze kutoa taarifa ya operesheni ya Jumatatu saa nne kuondoa vitendea kazi pamoja na biashara katika eneo la barabara wanayofanyia biashara.
Pia amesema alifanya jitihada za kumtafuta Diwani pamoja na Mkurugenzi wa Manispa kwaajili ya kuomba suluhu juu ya jambo hilo lakini juhudi hiizi hazikuzaa matunda…” Lakini Operesheni ya kutuondoa itaendelea kesho
Kwa Upande wa Mwanachama Musa Bin Rehan amesema kuwa kunafitina imeingia katika zoezi hilo, pia kunachoyo kimeingia juu ya chuki dhidi ya mwanadamu mwenziwe…. “Chokochoko na Kadhia zote zipo chini ya Awadhi ambaye ni msimamizi wa Msikiti baada ya kuamiwa na Bakhresa kusimamia mahitaji yeyote ya kigharama ya msikiti wa Mtoro lakini kinachoonekana mamlaka aliyopewa yamemlevya amefikia hatua ya kujiona mungu mtu.” Amesema