Samatta ashusha mjengo Masaki | Mwanaspoti

NAHODHA wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Mbwana Samatta ameshaonja mafanikio ya soka, lakini kama hujui nyota huyu anayekipiga PAOK ya Ligi Kuu ya Ugiriki amewekeza kwenye mambo mbalimbali ikiwamo mijengo Masaki, jijini Dar es Salaam.

Mmoja wa watu wa karibu wa nyota huyo aliyewahi kutamba na Simba, TP Mazembe kabla ya kutimkia KRS Genk ya Ubelgiji (hakutaka jina litajwe) alisema nyota huyo ni kweli amejenga ghorofa zilizopo Masaki kwa lengo la kupangisha watu mbalimbali.

Aliongeza sio tu ghorofa lakini nyota huyo amewekeza kwenye mambo mbalimbali nje ya soka miradi ambayo hapendi kuiweka wazi.

“Mimi mwenyewe nimekwambia tu lakini mwenyewe hapendi kuweka wazi vitu vyake, ni kweli Masaki amejenga ghorofa (Apartment) kwa ajili ya kupangisha watu mbalimbali ikiwemo wageni,” alisema.

Inaelezwa Samatta ameshusha mjengo huo ikiwa ni maandalizi ya kuelekea fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) ambayo Tanzania itakuwa mweyeji wa mashindano hayo ikiwa pamoja na Kenya na Uganda.

Lengo la Samatta ni kufanya biashara ya malazi kwani fainali hizo zinaleta wageni kutoka mataifa mbalimbali wakihitaji sehemu za kulala.

Related Posts