KIUNGO wa JKT Queens, Fatuma Bushiri ‘Tshishimbi’ amesema licha ya kucheza muda mrefu anapopata nafasi ya kuanza kwenye mchezo anapambana kuhakikisha timu inapata matokeo.
Mchezaji huyo amecheza kwa muda mrefu ligi ya wanawake akiwa Yanga Princess ambako alipata umaarufu kutokana na kuonyesa kiwango bora.
Mkongwe huyo alisema licha ya kukaa benchi anapopata nafasi ya kucheza anaonyesha kiwango bora ili kuisaidia JKT Queens ambayo ina malengo makubwa.
Tshishimbi aliongeza kinachomfanya aendelee kuwa na ubora ule ule ni nidhamu ya mchezo, kufanya mazoezi na maelekezo ya kocha.
“Siwezi kusema msimu mzuri sana kwa sababu ligi bado inaendelea, nikiingia huwa nafuata maelekezo ya kocha anaponiambia kama nikabe au kushambulia nafanya hivyo,” alisema nyota huyo.