ADEM YATUA GEREZA LA KIGONGONI BAGAMOYO KUTOA MSAADA KWA WAFUNGWA

NA VICTOR MASANGU,BAGAMOYO .

Katika kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita katika kuisaidia jamii   Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu-ADEM imeamua  kufanya ziara maalumu yenye lengo la  kutembelea wafungwa katika gereza la Kigongoni lilipo Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani na kutoa  misaada ya mahitaji ya msingi na vitu mbalimbali ambavyo vitawasaidia katika gereza hilo.

 Akizunngumza Katika ziara hiyo mkurugenzi wa taaluma wa ADEM Bugendi Joseph amesema  kwamba  wamepata  fursa ya kutembelea gereza hilo na kutoa mahitaji kama vile  miswaki, dawa za meno, viwembe, sabuni, unga na mchele  kwa kuzingatia mahitaji ya wafungwa.

Pia Bugendi amebainisha kwamba mbali na kutembelea gereza hilo pia  watumishi pamoja na wanafunzi wa ADEM wametembelea kituo cha kulelea watoto wanaotoka katika mazingira magumu cha  Amani Orphanage Center kilichopo katika Kata ya Zinga Wilayani Bagamoyo na kutoa msaada wa mahitaji  mbalimbali ikiwemo  vyakula, nguo, vifaa vya shule, na mahitaji mengine madogo madogo ya watoto wanaohudumiwa katika kituo hicho.

Aidha Mkurugenzi amesema  sambamba na kukabidhi msaada huo uongozi wa Adem ukaamua kuchangia  kiasi cha shilingi laki nane kwa ajili ya kuwasaidia katika  kuboresha mazingira ya nyumba yao wanayoishi hasa miundombinu ya umeme. 

Aidha, ziara hiyo pia imehusisha kutembelea Kaya zisizojiweza katika Kaya ya Kisutu, Bagamoyo ambazo zilibainishwa na Wenyeviti wa Mitaa katika Kata hiyo ambapo kaya zipatazo 13 zilisaidiwa mahitaji ya chakula na nguo.

Bugendi katika hatua nyingine amebainisha kwamba lengo la chuo hicho ni kuweka mikakati ya kuandaa wataalamu na viongozi mahiri ambao watakwenda kusaidia katika sekta ya elimu hapa nchini.

Naye Rais wa Serikali ya Wanafunzi-ASO Bw. Joshua Raphael  mara baada ya kukamilika kwa ziara hiyo amesema, wao kama wanachuo wa ADEM kwa kushirikiana na Menejimenti ya ADEM wanaona fahari kubwa kushirikiana na jamii inayowazunguka hasa kwa kuisaidia jamii katika mshitaji mbali mbali.

Adem imekuwa mstari wa mbele katika kufanya  Ziara kama hizo ambazo uwa zinafanyika  kila mwaka ili kurudisha huduma kwa jamii na mskundi mbali mbali  ikiratibiwa na Ofisi ya huduma saidizi za wanafunzi pamoja na Serikali ya Wanachuo wa ADEM-ASO.






         

Related Posts