Simba Queen yaongeza kipa Mkenya

SIMBA Queens imeanza mazungumzo ya kumpata kipa Wilfred Seda ukiwa ni ingizo la pili kwenye dirisha hili la usajili.

Mabingwa hao watetezi hadi sasa wamesajili kiungo Zawadi Khamis akitokea Fountain Gate Princess alipotoka Seda.

Mmoja wa viongozi wa Simba (jina tunalo) aliliambia Mwanaspoti wanaangalia uwezekano wa kumpata kipa huyo baada ya Carolyne Rufaa kukaa nje ya uwanja msimu mzima baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti.

Aliongeza, bado baadhi ya mambo hayajamilika kwani Jumatatu viongozi wa timu hiyo watakutana juu ya hatma ya mchezaji huyo anayekwenda kuongeza idadi ya makipa watatu wa Simba.

“Eneo la kipa ni muhimu sana, haikuwa na ulazima sana kwa sababu wapo wawili lakini hadi sasa bado hajasaini wanasubiriwa viongozi tu,” alisema kiongozi huyo.

Seda amecheza Fountain kwa misimu miwili tangu 2022/24 akiwa kipa namba moja wa timu hiyo na kama atasajiliwa ataongeza ushindani kwa Janet Shija na Gelwa Yona.

Related Posts