Mpina afyatuka bungeni, adai mawaziri wanampikia majungu

Dodoma. Mbunge wa Kisesa mkoani Mwanza, Luhaga Mpina amewatuhumu mawaziri kuwa wanampikia majungu kwa kuwa wameshindwa kujibu maswali ama hoja anazozitoa bungeni.

Mpina, ambaye amekuwa na kawaida ya kuzungumza bungeni na kuwachachafya mawaziri, amesema watendaji hao wa Serikali wameshindwa kujibu hoja zake na badala yake wamekuwa wakidai ana jambo lake.

Mpina ameyasema hayo leo Ijumaa, Mei 10, 2024 wakati akichangia mjadala wa kupitisha bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Maji kwa mwaka wa fedha 2024 / 2025.

“Nataka kuwaambia kwamba hakuna jambo lolote ambalo ninalo ila tuna jambo moja la Watanzania kupata maendeleo. Hakuna hiyana yoyote na huko wanakopeleka majungu, wengine wajue ndio tumekulia,” amesema Mpina.

Endelea kusoma mitandao ya Mwananchi kwa taarifa zaidi

Related Posts