Meneja wa Ritani kutoka Idara ya walipa kodi wa kati kutoka TRA, Sandey Kayombo akikabidhi zawadi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Suturn inayotengeneza magari aina ya Sinotruck, Chirag Tanna leo Desemba 23, 2024 walipotembelewa na Wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwaajili ya kuwashukuru na kusikiliza changamoto zao za kikodi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Suturn inayotengeneza magari aina ya Sinotruck, Chirag Tanna akizungumza leo Desemba 23, 2024 wakati walipotembelewa katika kiwanda chao na Wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwaajili ya kuwashukuru na kusikiliza changamoto zao za kikodi.
Meneja wa Ukaguzi kutoka Idara ya walipakodi wa Kati wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Haruna Myonga akipata maelezo walipotembelea kiwanda cha kuunganisha Magari cha Kampuni ya Suturn inayotengeneza magari aina ya Sinotruck.
Afisa Kodi kutoka Idara ya Walipa kodi wa Kati wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Rahma Mohamed akikabidhi zawadi kwa mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Bima ya Grand Re leo Desemba 23, 2024 walipotembelewa na Wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwaajili ya kuwashukuru na kusikiliza changamoto zao za kikodi.
Meneja wa Ritani kutoka Idara ya walipa kodi wa kati kutoka TRA, Sandey Kayombo akikabidhi zawadi kwa Mmoja ya wafanyakazi wa Kampuni ya Bima ya Grand Re leo Desemba 23, 2024 walipotembelewa na Wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwaajili ya kuwashukuru na kusikiliza changamoto zao za kikodi.
Mkurugenzi Mkuu Mtendaji kutoka Kampuni ya Bima ya Grand Re, Kuda Jeche akiwashukuru TRA kwa kufika katika ofisi zao kwa lengo la kuwashukuru kwa ulipaji kodi mzuri na kuwatakia heri ya Krismasi na Mwaka mpya katika Ulipaji wa Kodi.
MAMLAKA ya Mapato Tanzania kupitia Idara ya Walipakodi wa Kati leo Desemba 23, 2024 wamewatembelea na kuwashukuru Kampuni ya Suturn inayotengeneza magari aina ya Sinotruck na Kampuni ya bima ya Grand Re zilizopo jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Ritani kutoka Idara ya walipa kodi wa kati kutoka wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Sandey Kayombo akizungumza leo Desemba 23, 2024 wakati wa ziara ya kuwatembelea katika maeneo ya kazi walipa kodi hao amewashukuru yakwa kuwa walipakodi wazuri katika kipindi kilichopita.
Pia amewaomba kuwa na ushirikiano na Mamlaka hiyo katika kipindi kipya Cha miezi sita kinachokuja.
“Tumekuja hapa kwa mteja wetu, tukiwa kwenye mfululizo wa kuwashukuru walipa Kodi wetu ambao tumekuwa nao kwa kipindi Cha miezi sita wamekua na mchango mkubwa kwetu na wamekuwa na mchango mkubwa kwa taifa hivyo tumeona ni vyema kuja wakushukuru kwa mchango huo lakini pia kuwatakia heri ya krismasi na mwaka mpya.” Amesema Kayombo
Kwa Upande wa Mkurugenzi Mkuu Mtendaji kutoka Kampuni ya Bima ya Grand Re, Kuda Jeche amewashukuru TRA kwa kuwatambua katika kama ni walipaji wa wazuri kwani kodi.
Pia amesema TRA inakazi kubwa ya kufuta kumbukumbu ambayo ilikuwa inawafanya walipa kodi kuwaogopa na kuwakimbia pale tuu wanapowaona katika maeneo yao ya kazi.