UWANJA wa kikapu wa DB Osterbay unatarajiwa kuwaka moto wakati timu kongwe za kikapu nchini, JKT na Vijana (City Bulls) zitakapochuana kesho katika mchezo wa Ligi ya Kikapu ya Mkoa wa Dar es Salaam (BDL).
Mchezo huo unasubiriwa kwa hamu na wapenzi wa kikapu mkoani humo kutokana na upinzani mkubwa zilio nao timu hizo.
Timu ya Vijana inajivunia nyota wake, Fotius Ngaiza kutokana na uwezo wa kuchukua mipira ya ‘rebound’ na kufunga, huku JKT ikijivunia Baraka Sadick na Jonas Mushi ambao ni wafungaji wa maeneo ya mitupo mitatu.
Katika ligi hiyo mwaka jana, JKT iliifunga Vijana kwa pointi 76-60. Michezo mingine itakayochezwa uwanjani hapo leo ni Mchenga Stars itacheza na ABC, Mchenga Queens na Vijana Queens na wa mwisho utakuwa kati ya Pazi Queens na DB Troncatti.
Katika Uwanja wa Donbosco uliopo Upanga timu ya Kurasini Divas itacheza na Tausi Royals, Polisi Stars na Twalipo Queens, Kigamboni Queens na UDSM Queens na mchezo wa mwisho utakuwa kati ya DB Lioness na Ukonga Queens.
Wakati huohuo, Wachezaji Fotius Ngaiza wa Vijana (City Bulls) na Elias Nshishi wa ABC wanachuana vikali katika udakaji wa mipira (rebounder) katika Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL).
Ngaiza anayecheza nafasi ya ‘senta’ anaongoza baada ya kudaka mara 132 akifuatiwa na Elias Nshishi aliyedaka mara 131 Wachezaji wengine Elias Nshishi (ABC) mara 131, Jordan Jordan (Mchenga Stars 104), Amin Nkosa (Mchenga Stars 104) na Adam Lutungo (Mgulani JKT) mara 98.
Katika mchuano huo yupo pia Samwel Mwombe wa Dar City mwenye pointi 95, Cornelius Mgaza (Savio 94), Jimmy Brown (Outsiders 93), Haji Mbegu (Dar City 91) na Mwalimu Heri wa Outsiders 85.
Katika BDL mwaka jana, JKT iliifunga Vijana kwa pointi 76-60. Michezo mingine itakayochezwa uwanjani hapo leo ni Mchenga Stars itacheza na ABC, Mchenga Queens na Vijana Queens na wa mwisho utakuwa kati ya Pazi Queens na DB Troncatti.
Katika Uwanja wa Donbosco uliopo Upanga timu ya Kurasini Divas itacheza na Tausi Royals ilhali Polisi Stars na Twalipo Queens huku Kigamboni Queens na UDSM Queens zikiumana na mchezo wa mwisho utakuwa kati ya DB Lioness na Ukonga Queens.