NISHATI SAFI YA KUPIKIA YA RAFIKI BRIQUETTES YAACHA ALAMA TEMEKE

 

Shirika la Madini la Taifa STAMICO lafamya kampeni ya kutoa elimu na kuhamasisha  matumizi ya nishati safi nchini ili kuokoa mazingira na balaa la ukataji miti.

Akiongea kuhusu kampeni hiyo iliyofanyika Desemba  22, kwenye viwanja vya Mwembe Yanga  Wilayani Temeke Mstahiki  Meyaa wa Manispaa ya Temeke Ndugu Abdalla Mtinika ameipongeza STAMICO  kwa kushiriki moja kwa moja kuzalisha Nishati  safi na kuhamasisha matumizi  yake ili kuleta mabadiliko  kwa watanzania.

Amesema STAMICO  imepiga hatua mbele katika kufuata maelekezo ya Serikali  ya kwamba ifikapo Disemba 31, 2024 Taasisi zinahudumia watu zaidi ya 100 ziache kutumia nishati chafu na kugeukia nishati safi.

Amesema kwa kuleta Nishati hii STAMICO imefanya Mapinduzi yatakayoacha alama kwa kizazi kijacho kwa kuwa mazingira yatabaki kuwa salama kwa maisha ya watu

Ametoa shime kwa Serikali kuendelea kuwekeza kwenye mitambo ya uzalishaji ili kuipa Nguvu STAMICO  na kuiwezesha kuwa na kiwanda katika kila mkoa kwani hii itasaidia kuokoa idadi kubwa ya miti ambayo inateketea kwa kutengeneza nishati ya kupikia

Akiongea kuhusu Rafiki Briquettes Mkurugenzi Mtendaji  wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse amesema Chimbuko  la kampeni hii ya kuhamasisha ni kuunga mkono maono ya Serikali  ya kupunguza matumizi ya nishati zitokanazo na Miti na kugeukia nishati safi.

” Tumeona kuna haja ya kila mtanzania kushiriki kati suala la matumizi  ya nishati  Ndio  maana tukaja na kauli mbiu ya Zima Kuni na Mkaa  Washa Rafiki Briquettes” Alisema  Dkt.Mwasse 

Ametumia fursa hiyo kuwashukuru wadau wote wa STAMICO  wakiwemo mawakala na wanunuzi wa Rafiki Briquettes kwa kushirikiana  bega kwa bega na Shirika  hilo.

Ameongeza kuwa kampeni hizi zimeenda sambamba  utambuzi wa mawakala na utoaji Veti kwa mawakala  ili kuhakikisha mkaa huu umawafikia wengi 

Aidha, Mbunge  wa Viti Maalum wa Mkoa wa Dar es Salaam 

Mhe. Janeth  Masaburi ameishukuru Serikali  ya awamu ya sita kwa kuichukua ajenda hii ya dunia ya kulinda mazingira kwa kutumia nishati safi na salama.

Kwa upande wa watumiaji wa nishati hii Sajenti Yohana  Semwenda amesema  mkaa huu una manufaa kwa kuwa unadumu zaidi na umekuja kuondoa kabisa changamoto ya upatikanaji wa nishati ya kupikia.

 “Rafiki Briquettes  hii ni Rafiki  kweli kweli kimatumizi kwa kuwa  tangu tumeanza kutumia  tumeona  mkaa huu ni rafiki na salama kwani hauna moshi, unatumia mkaa mchache kupika chakula kingi na unawaka kwa muda mrefu.”

Amesema Semwenda

STAMICO imeenda kufanya kampeni hii Temeke ili wanatemeke waweze kuchangamkia fursa zinazotokana na nishati hiyo kushiki katika ajenda ya Kutunza mazingira.

Related Posts