WATANZANIA WATAKIWA KUJIANDIKISHA KWENYE KADI YA MPIKA KURA

Katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo mkoa wa Iringa MWL Joseph Ryata amewaomba watanzania kujitokeza kujiandikisha kwenye zoezi la kupata vitambulisho vya mpiga kura kwa ajili ya uchaguzi mkuu mwakani 2025.

Katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo mkoa wa Iringa MWL Joseph Ryata akipokea cheti cha shukurani baada ya mafunzo ya walimu Makada wa CCM mkoani Songwe

Na Fredy Mgunda, Songwe.

Katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo mkoa wa Iringa MWL Joseph Ryata amewaomba watanzania kujitokeza kujiandikisha kwenye zoezi la kupata vitambulisho vya mpiga kura kwa ajili ya uchaguzi mkuu mwakani 2025.

Akizungumza wakati wa mafunzo ya walimu Makada wa CCM mkoani Songwe, Ryata alisema kuwa moja ya jukumu kubwa la walimu ni kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi wajitokeze kujiandikisha kwenye vitambulisho vya mpiga kura.

Ryata alisema kuwa kila mwananchi anahaki ya kuhakikisha anajitokeza kupata kitambulisho cha mpiga kura ili katika uchaguzi ujao aweze kuchagua viongozi anaowataka kuwaongoza kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Alisema kuwa mwananchi asipokuwa na kitambulisho cha mpiga kura hatakuwa na haki ya kupiga kura kwa kiongozi yoyote katika uchaguzi mkuu mwakani 2025.

Nao baadhi ya walimu Makada wa CCM mkoa Songwe walisema kuwa wap tayari kuhakikisha wanatoa elimu kwa kila mwananchi kujitokeza kushiriki zoezi la kupata kitambulisho cha mpiga kura .

Related Posts