Mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe,Zakaria Mwansasu amesikitishwa na vitendo vya wanafunzi kudondoka mara kwa mara wakiwa shuleni huku vipimo vikishindwa kuonyesha ugonjwa unaowakabili na kupelekea jambo hilo kuhusishwa na imani kutokana na kukatwa kwa msitu uliokuwa ukitumika kwenye tambiko.
Akizungumza na wenyeviti wa vijiji pamoja na mitaa wakati wa semina elekezi kwa wenyeviti hao baada ya uchaguzi amesema katika shule ya msingi Uhenga pamoja na Uhekule zilizopo wilayani humo wanafunzi wamekuwa wakidondoka na vipimo vikishindwa kuonyesha ugonjwa wao.
“Shule ya msingi Uhekule watoto wanadondoka,tumejitahidi kuwahukua na kuwapima lakini wale watoto hawaumwi chochote na baaa ya kufuatilia kwa kina ni kwamba uliokuwa msitu wa kijiji umefyekwa na niko ulikuwa msitu wa tambiko sasa hii ni imani lakini watoto wanadondoka”amesema Mwansasu
Mwansasu amesema katika vijiji kuna wazee wenye mila na tamauni zao zisizovunja sheria hivyo wanao wajibu wa kuwasikiliza ili kuepuka changamoto pamoja na kwena kusimamia kwa kuyatunza na kuhuisha misitu iliyopo vijijini
“Tunao waze katika vijiji vyetu ambao wana mila na tamauni zao lakini hizi mila na tamauni zao hazivunji sheria wakikwambia hili pori sio la kuuza wala sio la kukata kuni liache,wakikwambia huu mti hapa sio wa kuutoa uache”aliongeza Mwansasu