WATUHUMIWA Watano Wakiwemo Raia Wa China Wawili Wanaokabiliwa na Tuhuma za Kuharibu Miundombinu Ya Reli Ya Kisasa (SGR) Wamepandishwa Kwa Mara ya pili Katika Mahamakama ya Wilaya ya Kibaha Wakikabiliwa na Makosa Sita Yakiwemo Matano ya Uhujumu wa Miundombinu Ya Reli na Utakatishaji wa Fedha.
Akiwasomea Mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Wa Mahaka hiyo Mheshimiwa Felister Ngh’welo ,Mwendesha Mashtaka wa Serikali Daudi Sabaya amesema Watuhumiwa Wanadaiwa Kutenda Makosa hayo Katika Nyakati tofauti Kati ya Mwezi Novemba na Disemba 2024 Katika Eneo la Miwaleni Mlandizi Mkoa Wa Pwani .
Mwendesha Mashtaka huyo amewasomea Mashtaka yao Watuhumiwa Wang Long Yu (62) Raia wa China, Zang Dong Feng (55) Pia Raia wa China ,Pius Kitulya (53) Raia Wa Nchi Jirani ,Paul Joseph John (30) Mtanzania Na Abduli Mohamed Mboya pia Mtanzania ,ambapo Amesema Katika Nyakati tofauti Walipatikana na Mali zinazodhaniwa za Wizi Mali ya Shirika la Reli Tanzania, Ikiwmeo Lilo 1,152.4 na Kuitia Hasara TRC Ya Shilingi zaidi ya Milioni 217.
Aidha Watuhumiwa Hao Katika Nyakati tofauti Maeneo Ya Mlandizi Wamedaiwa Kukamatwa na Polisi Wakiwa na Kilogramu 882.5, Kilogramu 263,Kilogramu 1,152.4 ,Kilogramu 6.4 za Waya Wa Kopa na Waya Wa Kupitishia Umeme Kwenye Treni (CATERNARY) Mali ya TRC isivyo Halali.
Hakimu Mkazi Wa Mheshimiwa Felister Ngh’welo aliwaambia Watuhumiwa Hao Kuwa Hawatakiwi Kujibu chochote Kwa Kuwa Mahakama hiyo Haina Mamlaka ya Kusikiliza shauri hilo,ambapo amesema litatajwa Januari 06,2025 ,Kufuatia Kutokamilika Kwa Upelelezi Kwa Mujibu wa Mwendesha Mashtaka wa Serikali hatua iliyolazimu Watuhumiwahso Kurejeshwa Mahabusu Kufuatia Kukamilika Kwa Mujibu Wa Mwendesha Mashtaka Wa Serikali hatua iliyolazimu Watuhumiwa hao Kurejshwa Mahabusu Kufuatia Tuhuma dhidi yao Kutokuwa na Dhamana.
Katika Hatua Nyingine Wakili anayewatetea Watuhumiwa Nambari 1,2,3 na 5 Nestory Wandiba Wake, aliiambia Mahakama hiyo Kuwa Wateja Wake Wamekubali Kuandika Hati Ya Kukiri Kosa, Hata Hivyo Mahakama iliamuru Waendelee na Mchakato huo Kwakuwa Uko nje ya Wigo wa Mahakama na Kwamba itapokea Kitakachozungumzwa na pande Mbili hizo.Kesi hiyo ilisomwa Kwa Mara ya Kwanza Disemba 20,2024 ambapo Watuhumiwa Walisomewa Mashtaka Matano ya Uhujumu WA Miundombinu Ya Reli Kabla ya Serikali Kuongeza Kosa Utakatishaji fedha.