Wanne wafariki kwa shoti ya umeme msibani

Handeni. Watu wanne wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa baada ya kupigwa na shoti ya umeme wakati wakifunga maturubai msibani Mtaa wa Ngugwini, Halmashauri ya Mji wa Handeni mkoani Tanga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi amesema tukio hilo limetokea leo Jumanne saa 3:40 asubuhi katika mtaa huo.

“Waliofariki dunia katika tukio hilo ni  Fredy William Mwangunda (43), Mhina Athuman Mangagwa (35), Andrew Allen Mkomwa (29) na Salehe Omary Machaky (25) aidha, majeruhi ni William Gumbo (50) na Mbega Ally (49),”amesema Kamanda Mchunguzi.

Mkazi wa Handeni Omari, amesema watu walipumzika kwa ajili ya kusubiria shughuli ya mazishi, lakini ukatolewa utaratibu wa kutenga maturubai kuyasogeza upande mwingine.

Endelea kufuatilia Mwananchi.

Related Posts