NA WILLIUM PAUL, SAME.
MVUA zinazoendelea kunyesha wilayani Same mkoani Kilimanjaro zimesababisha kukatika kwa daraja ya Kizangaze na kukata mawasiliano ya kati ya kata ya Maore, Ndungu, Kihurio, Bendera na kata ya Miamba kwa takribani saa 72 sasa.
Mbali na kukatika kwa mawasaliano hao, pia zimesababisha vifo vya watu sita wakiwemo wawili wa familia moja huku baadhi ya wananchi wakiachwa bila makazi baada ya nyumba zao kuangukiwa na ngema.
Wakizungumza jana baadhi ya wananchi akiwemo Loveness Julias alisema mvua hizo zimechangia kupotezwa kwa ndugu zao pamoja kusombwa kwa mazao shambani.
“Hatuna mawasiliano toka juzi, wasafiri wameshindwa kusafiri, maiti zinavushwa kwenye maji kwa shida,hakika ni adha kubwa, hasa msimu wa mvua,”alisema Ally Yusufu.
Naye diwani kata ya Maore, Rashid Juma, alisema kutoka kwa daraja hilo kumesababisha wananchi kutembea zaidi ya kilomita 60 kufuata huduma za Afya katika hospitali ya Wilaya ya Same badala ya kilomita tatu kituo cha afya cha Ndungu.
“Kwa sasa watu tunakabiliwa na matatizo mengi, yakukosa usafiri kwenda kituo cha afya, kupeleka mazao sokoni.huko ndiko iliko sheli (kituo cha mafuta) kikubwa ambacho tunanakitegemea,
Baadhi ya abiria waliokwama ni wa kwenda Dar, Tanga Morogoro lakini kwa sasa ili uende huko nilazima urudi Same ndipo uanze safari na nauli zimepanda hasa kipindi cha mwisho wa mwaka,”alisema Juma.
Alisema kukatika kwa daraja hilo sio mara ya kwanza kukatika na kuiomba serikali kuangalia suluhisho la kudumu.
Akitoa jitihada za kazi wanazofanya Kaimu Meneja wa wakala wa barabara
(TANROADS) mkoa Kilimanjaro Mhandisi Benitho Mdzovela alisema katika jitiada za awali kurudisha mawasiliano hayo, wameweka pipu calvati za plastiki tatu kila moja linakipenyo cha mita moja na nusu.
Alisema zitasidia kupitisha maji kwa dharura na baadaye wanatarajia kujenga daraja la kudumu kutokana na daraja hilo kuwa la zamani.
“Mvua zimesababisha kukatika kwa mawasaliano kwa kuvunja kutangumu za daraja, kwa sasa tunategemea kutumia milion zaidi 30 na mawasiliano yatarejea baadaye ya siku mbili.
Aidha alipotembelea daraja hilo na kujionea hali halisi ya uharibifu, Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu alitoa mkono wa pole wa kiasi cha milion tatu na kuwataka wananchi kuondoka maeneo hatarishi.
“Nawaagiza viongozi wetu kwanzia ngazi ya kijiji hadi wilaya kuaishisha maeneo hatarishi na kuwashawishi wananchi kuondoka maeneo hayo ili kuepuka wadhara yanayoweza kutokea hasa ya vifo na uharibifu wa mali.,”alisema Babu.