JAMII YAASWA KUWAKUMBUKA WENYE MAHITAJI MAALUM KIPINDI CHA SIKUKUU ZA MWISHO WA MWAKA.

Na WMJJWM-Dar Es Salaam

Jamii imehimizwa kuwakumbuka watu wenye Mahitaji Maalum katika msimu huu wa Sikukuu kwa kuwapatia zawadi na mahitaji mbalimbali ili waweze kusheherekea kwa furaha Sikukuu za mwisho wa mwaka.

Rai hiyo imetolewa Desemba 25, 2024 na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake Jinsia na Wanawake na Makundi Maalum, (anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii na Makundi Maalum) Wakili Amon Mpanju wakati akikabidhi zawadi mbalimbali kwa watoto wanaolelewa katika Makao ya ya Taifa ya Watoto Kurasini Dar Es Salaam, kwa niaba ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

“Msimu wa Sikukuu jamii inapaswa kuwakumbuka na kuwasaidia watu wenye mahitaji Maalum kama wezee na watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi ni jambo la baraka na linatoa matumani Kwaao na kujiona ni kama watu wengine” amesema Wakili Mpanju.

Aidha Wakili Mpanju ametoa wito kwa Mashirika, Taasisi za Serikali, Mashirika yasiyo ya Kiserikali na jamii kuhakikisha watoto, wazee na watu wenye mahitaji Maalum wanasherehekea kwa furaha Sikukuu za mwisho wa mwaka kwa kuwakumbuka kwa zawadi na mahitaji mbalimbali ya kibinadam.

Kwa upande wake Makamu Mfawidhi wa Makao hayo Farida Ismael amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa zawadi hizo ambazo zitawasaidia watoto kula na kunywa na kufurahia sikukuu za mwisho mwaka kama watoto wengine.

Naye mmoja wa mtoto anayelelewa katika Makao hayo Festo Elias kwa niaba ya watoto wenzake amemshukuru Rais Samia kwa kuwakumbuka watoto katika kipindi hiki cha Sikukuu na ameeleza kufurahia zawadi hizo na kuomba wadau na taasisi zingine kufanya hivyo mara kwa mara.

Related Posts