ISSA GAVU ATOA ZAWADI KWA WASHINDI WA MASHINDANO YA MICHEZO MBALIMBALI – UNGUJA

Mwakilishi wa Jimbo la Chwaka Mkoa kusini Unguja Mhe. Issa Ussi Gavu ambaye ni Katibu wa Oganazesheni wa CCM Taifa (MCC) ametoa zawadi mbalimbali za medali, vikombe na fedha kwa washindi walioshinda kwenye mashindano ya waendesha baiskeli, mchezo wa bao, karata, kukimbiza kuku nk.

Kabla ya kuanza kwa mashindano hayo wananchi wa Jimbo hilo na viongozi mbalimbali wa Chama walianza kwa matembezi ya amani kuhamasisha kuelekea miaka 61 ya sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar ambayo yanatarajiwa kufanyika mwezi Januari 12 mwaka 2025.

Wakizungumza kwenye tamasha hilo wananchi hao wameshukuru Serikali ya CCM Chini ya Rais Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi na Mwakilishi wa Jimbo hilo kwa kuwaletea maendeleo na kutimiza zaidi ya asilimia 95 ya ahadi zake katika kipindi cha muda wake wa uongozi na kutekeleza ilani ya CCM ikiwemo barabara, afya, elimu na fursa za uchumi kwa vijana na wanawake.

Mashindano hayo yamefanyika ikiwa ni kuelekea miaka 61 ya sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar.











Related Posts