Tisa wafariki dunia ajali ya basi, Noah Rombo

Rombo. Watu tisa wamefariki dunia katika Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro baada ya gari dogo aina ya Toyota Noah kugongana uso kwa uso na basi la abiria Kampuni ya Ngasere.

Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Raymond Mwangwala amethibitisha kutokea ajali hiyo leo Alhamisi Desemba 26, 2024 ambapo amesema miili hiyo imepelekwa Hospitali ya Karume, wilayani humo.

Mwangwala amesema majeruhi mmoja ambaye amesalia katika ajali hiyo amepelekwa hospitali ya Huruma kwa matibabu zaidi.

“Kwenye Noah tumetoa miili tisa na yote tumeihifadhi Hospitali ya Karume, na majeruhi mmoja amepelekwa Hospitali ya Huruma,” amesema.

Mwangwala amesema chanzo cha ajali hiyo ni baada ya gari aina ya Noah lililokuwa likitokea Tarakea kulipita Fuso na kwenda kugongana uso kwa uso na basi la Ngesere lililokuwa likitokea Dodoma kuja wilayani humo.

Related Posts