Kocha wa Timu ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes, Hemed Suleiman ‘Morocco’ amewaondoa kambini nyota wake wawili kwa utovu wa nidhamu.
Katika taarifa iliyotolewa na ZFF, nyota waliofukuzwa ni Ibrahim Mkoko anayekipiga katika klabu ya Namungo FC na Abdallah Said (Lanso) wa KMC.
Utovu wao wa nidhamu uliotajwa katika taarifa hiyo ni kuchelewa kujiunga na kambi ya timu ya Taifa inayojiandaa na mashindano ya Mapinduzi Cup yanayotarajiwa kuanza rasmi Januati 3, 2025 msimu huu yakihusisha timu za Taifa, ikiwa tayari walisharuhusiwa na klabu zao.
Aidha, Morocco amemuongeza Ali Juma Maarifs (Mabata) anayekipiga kwenye kikosi chA Uhamiaji inayoshiriki Ligi kuu Zanzibar.
Heroes iliingia kambini Desemba 24 na jana ilianza rasmi maandalizi.