Wananchi Ngombo – Malinyi waomba zoezi kuwahamisha lisitushwe

Wananchi wa Kijiji cha Ngombo Wilaya ya Malinyi Mkoani Morogoro wemeiomba Serikali ya Wilaya hiyo kusitisha zoezi la kuwaondoa katika Kijiji hicho Ili kupisha hifadhi ya Pori la Akiba la Kilombero, kwani baadhi Yao bado hajalipwa fedha za fidia huku wengine wakidai kupewa muda mchache wa kuhama pamoja kushindwa kuwatengea eneo la maalum la kwenda kuishi.

Wakizungumza na Kituo hiki baadhi ya Wananchi hao akiweno Wilbroad Choga amesema utaratibu wa kuhamishwa katika Kijiji hicho haukufuata makubaliano Yao ya kuwatengea eneo maalum la.kwenda kuishi jambo kusababisha kulala nje zaidi ya siku nne wasijue wapi wataelekea .

“unapewa fedha Leo kesho unaambiwa uhame hawajutengea eneo ka Kwenda kuishi sehemu zote za kutokea Huduma zote zimefungwa maduka,shule , Hospital tunaomba Serikali itusaidie ” Wilbroad Choga mkazi wa Kijiji Cha Ngombo.

“wengine hatujalipwa pesa tunaambiwa tuhame pesa zitatufuata hukokuko je mzigo yetu tunabebea Nini”

Kutokana na changamoto hiyo kituo hiki kimemtafuta Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Sebastian Waryuba ambapo amekili kushindwa kuwatengea eneo Wananchi wanaohama katika Kijiji hilo ambapo Serikali imetoa uhuru kila mwananchi aende sehemu yeyote anayohitaji na kuhusu suala la malipo amesema zoezi linaendelea kuwapatia fedha watu ambao bado hajalipwa.

Amesema zaidi ya shilingi Bili 7.3 zimetengwa Kwa ajili ya kuwalipa fidia wakazi hao kwenye kaya zaidi ya 1000 wa eneo hilo Ili kupisha hifadhi .

DC Waryuba amesema zoezi la kuwataka wananchi hao kuhama haraka ni kutokana changamoto ya jiografia kwani Kijiji hicho kimezungukwa na mito mikubwa ambayo inasababisha mafuriko.

“ndugu mwandishi kule kama ulivyokuona Kijiji kipo kisiwani kimezungukwa na mito mikubwa Miwili Sasa ukiacha Kuhama mwezi huu itabidi usubiri Hadi mwezi wa sabaa au wa nane mvua ziache kunyesha sasa Serikali haitakuwa na pesa nyingine ya kuwalipa fidia mazao Yao”Dc Waryuba.

 

 

Related Posts