Jinsi ya kutumia chakula kama dawa ya kisukari

Kwa wagonjwa wa kisukari, kutumia chakula kama dawa ni njia mojawapo ya kudhibiti kisukari na kupunguza madhara ya ugonjwa huu. Mlo sahihi unaoweza kudhibiti viwango vya sukari unaweza kuepusha madhara ya kisukari.

Matumizi ya vyakula vyenye makapimlo ua ‘fiber’ kama matunda, mboga za majani, nafaka isiyokobolewa na wanga aina ya mizizi kama maboga, vyakula vya protini kama maharage, mbaazi.

Ulaji wa vyakula vya wanga asili, nafaka ambayo hajakobolewa kama unga wa ngano na unga wa mahindi ambayo hayajakobolewa, shayiri, mchele wa rangi ya hudhurungi pia zinaweza kusaidia kuthibiti sukari.

Epuka vyakula vyenye sukari ya ziada kama keki, juisi za viwandani na vyakula vyote vyenye sukari ya kuongezwa vinaweza kuongeza viwango vya sukari kwenye damu kwa haraka.

Vyakula hivi vinaweza kuchangia katika kuongezeka kwa uzito na matatizo ya kisukari, hivyo ni muhimu kuviepuka.

Wagonjwa wa kisukari wanapaswa kuepuka matumizi ya mafuta yanayotokana na wanyama na kuanza kutumia mafuta ya mimea kama mafuta ya mizeituni, mafuta ya alizeti na mafuta ya parachichi na karanga.

Pia mafuta ya ubuyu au mafuta ya samaki (omega-3). Mafuta haya husaidia kudhibiti viwango vya sukari kwenye damu na kuboresha afya ya moyo.

Matunda na mboga za majani ni chanzo kikubwa cha vitamini, madini na fiber ambayo ni muhimu kwa udhibiti wa kisukari. Matunda yenye sukari ya asili kama tufaa, madalanzi na parachichi yanaweza kuliwa kwa kiasi, lakini ni muhimu kuepuka kula kwa wingi matunda yanayoongeza sukari haraka kwenye damu kama vile zabibu na mananasi.

Kunywa maji ya kutosha husaidia kudhibiti viwango vya sukari kwenye damu kwa kuongeza uwezo wa figo kutokomeza sukari kupita kwenye mkojo.

Pia maji husaidia kudhibiti uzito, jambo muhimu katika kudhibiti kisukari. Unywaji ya kutosha inasaidia kuondoa sumu mwilini na kudhibiti viwango vya sukari.

Ulaji wa vyakula vyenye madini ya magnesium ni muhimu kwa sababu yanahusiana na ufanisi wa insulin na udhibiti wa viwango vya sukari. Vyakula vyenye magnesium ni kama mbegu za maboga, maharage na spinach.

Kama una kisukari, jitahidi sana kutumia vyakula na kula mlo sahihi kama dawa ya kudhibiti viwango cha sukari, hii ina maana kuwa unatakiwa kula vyakula sahihi na vyenye makapimlo au fiber ya kutosha, kufanya mazoezi ya mara kwa mara, kuepuka msongo wa mawazo, kuhudhuria kliniki ya kisukari mara kwa mara ni muhimu pia.

Related Posts