Abdulaziz Makame afukuzwa kambini, Heros kwa utovu wa nidhamu

Kocha wa Zanzibar Heros, Hemed Suleiman Morocco amemfukuza kambini beki Abdulaziz Makame (Bui) kwenye kambi ya kikosi hicho kinachojiandaa na mashindano ya Mapinduzi Cup yanayotarajiwa kuanza Januari 03, 2025 kisiwani Pemba.

Katika taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF) imesema Bui amefukuzwa kambini kwa utovu wa nidhamu baada ya kushindwa kuripoti mapema kambini ikiwa alipataruhusa mapema ya kujiunga kwenye kikosi cha Heros katika klabu yake ya Geita Gold.

Hata hivyo Morocco amemuongeza kikosini, Abubakar Nizal wa Azam FC U20 na Abdul Nasir Mohamed Abdallah ‘Casemiro’ wa Mlandege FC.

Makame anakuwa mchezaji wa tatu kuondolewa kwenye kikosi hicho baada ya awali kuondolewa nyota wawili Abdalah Said (Lanso) anayekipiga KMC na Ibrahim Mkoko anayekipiga Namungo FC.

Heros iliingia kambini Desemba 24, 2024.

Related Posts