Mamlaka ya mapato Tanzania TRA Mkoa wa Tanga imewatembelea na kutoa shukrani kwa walipa Kodi upande wa Shule za sekondari wilayani Lushoto Mkoani hapa.
Akizungumza mara baada ya kuwatembelea walipa Kodi wa Shule ya Sekondari Mazinde Juu na Shule ya Sekondari Kifungiro Girl’s Naibu Kamishna Huduma wa za Kiufundi TRA Bw.TedFrank Sirlikuwasha ambaye amemwakilisha Kamishna Mkuu Bw.Yusuph Mwenda amesema kuwa wanawatembela walipa Kodi Ili kuchukua changamoto ambazo wataziboresha wakati wa ukusanyaji wa kodi.
“Tunapowatembelea hawa walipakodi kuwa wao ni washindi Kodi zetu zinalipika kwani unalipia Kodi huku unaendelea kufanya biashara Shule ya Kifungiro na Mazinde ni shule bora ambazo bado zinaendelea licha ya kuendelee kulipa Kodi ambapo Kamishna Mkuu ameona wanaochokifanya kinatambulika na kinamchango Kwa Serikali”
Kwa upande wa Shule ya wasichana ya Kifungiro kupitia Mkuu wa shule msaidizi Sister Pia Shayo amesema kuwa wameishukuru uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Kwa kuwatembelea na kuwaheshimisha Kwa kuwapatia zawadi kwasababu ya ulipaji wa Kodi.
“Mimi kama mdau napenda kusema ni vizuriwatu wote wenye sekta kama hiiambazo kiuchumi tunatakiwa tuchangie tuwe mfano wa kulipa Kodi maan asyo kubwa Kwa ajili ya Maendeleo ya Taifa” .
Naye Mkuu wa shule ya Mazinde Juu Sister Eveta Kiramba ameshukuru Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kutambua mchango wa shule Mazinde Juu kwa uaminifu wa ulipaji wa kodi.
“Tunajitahidi kwasababu tunatambua ni wajibu tutaendelea kufanya hivyo wetu wa ulipaji wa Kodi na kufanya kazi na TRA ni kuisupport Serikali yetu kwani shule hii inamilikiwa na Jimbo Kuu katoliki Tanga”.
Wakati huo huo mamlaka ya mapato Tanzania TRA iliwatembela wafanyabiashara wa Vinywaji ikiwepo Magpie Distributors ambapo Mkurugenzi wake Bi.Mary Makoi amesema kuwa wanashukuru mamlaka ya mapato Tanzania TRA kwa kuthamini mchango wao na kuwaona na kuwapatia zawadi ambapo itawapa motisha zaidi katika ulipaji wa Kodi.
Aidha Naibu Kamishna wa huduma za Kiufundi Tedfrank Sirlikuwasha anawakumbusha walipa Kodi kulipa Kodi Kwa wakati Ili kumaliza mwaka na kutimiza malengo yaliyowekwa na Serikali.