Wawili wadakwa kwa kuingia vipodozi vyenye sumu

 

JESHI la Polisi Mkoa wa Songwe linamshikilia watu wawili kwa tuhuma ya kusafirisha vipodozi vyenye viambata vya sumu aina mbalimbali boksi 201. Anaripoti Mwandishi Wetu, Songwe … (endelea).

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe, SACP Augustino Senga amewataka watuhumiwa hao ni dereva wa lori tenki la mafuta lenye namba za usajili T.747 DDE na tela namba T.330 CJX aina Ya FAW TANK, Jackson Wilson Kashebo (45) mkazi wa Mbagala Dar es Saalam na utingo wake, William Fillickson Sichone (34) mkazi wa mtaa wa Chapwa Wilaya ya Momba.

Wawili hao |walikamatwa tarehe 28 Desemba, 2024 majira ya saa 11:15 asubuhi huko mtaa wa Keseria kata ya Chapwa Wilaya ya Momba, baada ya Jeshi la Polisi mkoani hapa kupata taarifa za siri na kuweka mtego uliofanikisha kuwatia mbaroni watuhumiwa wakiwa wamepakia na kusafirisha shehena ya vipodozi vyenye viambata vya sumu boksi 201 kwenye vyumba vya kubebea mafuta aina ya Petrol/Disesel wakitokea nchini Kongo na kuingiza nchini.

Vipodozi walivyokamatwa ni:- Extra clair box 30, Betasol tube box 14, Pawpaw cream 64, Snail white Box 16, Prety white box 8, Extra clair lemon box 27, Bronz tone box 8, Clear therapy box 14, Parfect white box  8, Cocopup water box 12, Esapharm movete Pcs 230 na Esapharma lemonvate Pcs 160.

Aidha katika mwendelezo wa operesheni na msako huo Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe likishirikiana na wataalam kutoka TFRA na Halimashauri ya Mji Tunduma limewakamata watuhumiwa 2 ambao ni Gosso Sadick Mussa (32) na Prisca Filipho Shembe (37) wote wakazi wa Sogea Tunduma wakiwa na mifuko 125 iliyofungashwa bila kibali ikiwa ni pamoja na kuuza mbolea nje ya bei elekezi na kufanya udanganyifu wa kuuza mbolea ya DAAP Plus kampuni ya Minjingu iliyofungashwa kwenye mifuko ya DAP kampuni ya FALCON ETG, pia watumiwa hao walikutwa na mashine ya kushonea mifuko hiyo ambayo ni POTABLE BAG SEALING MACHINE pamoja na mifuko tupu mipya 153 ya kampuni mbili tofauti.

Tukio hili limetokea Disemba 28, 2024 majira ya saa 02:00 asubuhi huko mtaa wa Unyamwanga kata ya Tunduma Wilaya ya Momba na kuikuta mifuko hiyo imefichwa kwenye ghala la kuhifadhia bidhaa mbalimbali za pembejeo kwa lengo ya kuiuza. Upelelezi wa shauri hili bado unaendelea na watuhumiwa wote wanne watafikishwa mahakamani pindi upelelezi utakapokamilika.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linatoa wito kwa jamii kuachana na biashara haramu/magendo, usafirishaji na uingizaji wa bidhaa zilizopigwa marufuku nchini kwani zinasababisha madhara kiafya kwa watumiaji. Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linaendelea kuwahakikishia wananchi kuwa,  lipo makini na imara katika kuhakikisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao, halitasita kumkamata wala kumuonea muhari mtu yeyote atakayebainika kujihusisha na uhalifu.

About The Author

Related Posts