WAFANYABIASHARA, JAMII INAYOJIHUSISHA NA SEKTA YA MADINI WATAKIWA KUHAKIKISHA WANATUMIA VIFAA VYENYE UBORA

Na Mwandishi wetu

Wafanyabiashara wa madini pamoja na jamii inayojihusha na sekta ya madini wametakiwa kuhakikisha wanatumia vifaa vyenye ubora katika uchakataji wa madini ili kuongeza ubora kwa ustawi wa shughuli za madini na kuendana na kasi ya maendeleo ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Nesch Mintech Tanzania Limited Happiness Nesvinga, amesema mchakato mzima wa kuanzia kuchimba mpaka kuuza madini ni mkubwa lakini jambo linaloongeza thamani yake zaidi na kumlipa mfanyabiashara ni pale ambapo madini hayo hupimwa na kuhakikiwa katika ubora wa juu na kuepuka makosa ya gharama kubwa na kudumisha ushindani.

“Huduma za maabara ni muhimu kwa mafanikio na ustawi wa operesheni za madini. Hivi ndivyo tunavyofanya kazi zetu. Nesch Mintech, tunajivunia taratibu zetu nzuri za upimaji. Tunachambua sampuli za madini katika kila hatua ya uchakataji ili kuhakikisha kuwa bidhaa ya mwisho si tu inakidhi bali inazidi viwango vya sekta. Kujitolea kwetu kwa ubora kunasaidia wateja,” amesema Happiness.

Ameongeza kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amewekeza zaidi katika Kuboresha Michakato ya Uchimbaji na kampuni ya Nesch Mintech ina Maabara ambayo imejengwa na teknolojia ya kisasa ili kutoa data sahihi kwa ajili ya uboreshaji wa michakato na inasaidia makampuni ya madini kutambua njia za uchimbaji zenye ufanisi zaidi, kupunguza gharama za uendeshaji na kuongeza uzalishaji.

Aidha Uwajibikaji wa mazingira katika shughuli za madini ni kiini cha operesheni zote na inatakiwa vipimo kamili ili kufuatilia athari za shughuli za madini, kuwasaidia wateja wetu kufuata kanuni za mazingira na kulinda sayari nzima kwa vizazi vijavyo.

Happiness ameongeza kuwa, Nesch Mintech ni kituo cha utafiti na maendeleo ambacho mara kwa mara kinatafuta mipaka mipya katika mbinu za uchimbaji na uchakataji madini, kuchangia katika maendeleo ya kiteknolojia katika sekta ya madini na kutathmini uwezo wa kiuchumi wa amana za madini kwa kuhakikisha faida ya miradi ya madini.

Rai kubwa ya Mkurugenzi huyo kwa wafanyabiashara wa madini ni kuweka kipaumbele kwa Usalama katika shughuli za madini. “Tunapima kwa makini hatari zinazowezekana, kuhakikisha ustawi wa wafanyakazi wa migodi na jamii zinazozunguka. Huduma zetu za maabara ni muhimu kwa kuunda mazingira salama ya kazi.”

Nesch Mintech Tanzania Limited ni zaidi ya maabara imekuwa ni washirika katika maendeleo na inaunga mkono serikali katika sekta ya uchakataji madini, kuhakikisha kuwa operesheni za madini ni zenye ufanisi, zinawajibika, na zina faida kwa kuwahakikisha utaalamu usio na kifani na msaada usioyumba.






Related Posts