Adhabu zaipa bodi ya ligi Sh10.5 milioni

Adhabu mbalimbali zilizotolewa na kamati ya uendeshaji na usimamizi ya bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB)  kuvuna Sh10.5 milioni.

Adhabu hizo zimetokana na makosa mbalimbali yaliyofanywa na timu, wachezaji, viongozi na maofisa wa timu za Ligi Kuu, Ligi ya Championship na First League.

Kiasi kikubwa cha fedha kimetozwa kwa Biashara United ya Mara ambayo imetakiwa kulipa faini ya Sh3 milioni kwa kosa la kushindwa kufika uwanjani katika mechi ya ligi ya Championship dhidi ya Mbeya City iliyokuwa ichezwe Desemba Mosi, 2024.

Mbuni FC imetozwa Sh2 milioni kwa makosa mawili ambayo kila moja adhabu yake ni faini ya Sh1 milioni nayo ni mchezaji wake Pascal Mwakapusya kumpiga refa msaidizi na pia mashabiki wake kumfanyia vurugu refa huyohuyo Leah Petro.

Faini nyingine ni Sh1.5 milioni kwa meneja wa KenGold, Nuhu Nkaekwa, Sh1 milioni kwa kocha msaidizi wa Azam FC, Bard Eddine Dris, Sh 500,000 kwa JKT Tanzania, Sh1.5 milioni kwa kocha wa makipa wa Geita Gold, Augustino Malindi Sh1 milioni kwa kocha wa African Lyon, Elia James na kocha wa makipa wa African Lyon Ibrahim Bigambo.

Kamati hiyo pia imetoa onyo kali kwa mtendaji mkuu wa JKT Tanzania, Jemedari Said kwa kosa la kuingia uwanjani katika mechi dhidi ya Simba onyo ambalo pia limetolewa kwa Abdihamid Moalin wa Yanga.

“Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania imempa Onyo Kali Mkurugenzi wa Ufundi wa klabu ya Yanga, Abdihamid Moallin kwa kosa la kuketi kwenye benchi la ufundi la klabu hiyo katika michezo mitatu (3) ya Ligi Kuu ya NBC kinyume na matakwa ya Kanuni ya 17:17 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

“Adhabu hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 17:62 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za

“Aidha, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania inautaarifu umma kuwa imepokea taarifa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuwa klabu ya Yanga imekamitisha taratibu zote za kumtumia bwana Abdihamid Moallin kama kocha msaidizi namba mbili wa kikosi chao na ataanza kutambuliwa kikanuni katika mchezo wa leo Desemba 29, 2024 dhidi ya Fountain Gate,” imefafanua taarifa ya kamati ya uendeshaji na usimamizi wa ligi ya TPLB

Related Posts