WAZIRI MKUU MSTAFU MIZENGO PINDA APONGEZA UTEKEKEZAJI MRADI WA HEET CHUO KIKUU SUA

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda amefanya ziara katika Ndaki ya Kampasi ya Mizengo Pinda, Mkoani Katavi ikiwa ni mojawapo ya Kampasi za SUA kwa lengo la kujionea shughuli za maendeleo chuoni hapo.

Mhe. Mizengo Pinda amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada anazofanya za kuinua elimu na uchumi kwa wananchi katika mkoa wa Katavi, kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi ambao utachochea maendeleo ya Chuo, mkoa na wananchi kwa Ujumla.

Pia Mhe. Pinda ameishukuru Menejimenti ya SUA kwa ujumla na kusema ana imani kupitia kukamilika kwa ujenzi huo utachochea ongezeko kubwa la wanafunzi na Shahada mbalimbali zitakazochochea mabadiliko ya kiuchumi katika eneo hilo na mkoa kwa ujumla.

Mhe. Pinda amesema hayo alipokuwa akizungumza na watumishi pamoja na wanafunzi katika ziara yake na mwisho alipata nafasi ya kwenda kujionea maendeleo ya mradi unaofanywa na kampuni ya Til Construction.





Related Posts