TABORA UNITED KUWAKARIBISHA MASHUJAA FC KESHO MWINYI




Kikosi cha Timu ya Tabora United kesho kitashuka  katika Uwanjawa wa  Ali Hassan Mwinyi kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC soka Tanzania Bara dhidi ya Mashujaa FC ya Mkoani Kigoma  utakaochezwa saa nane kamili mchana. 


Nyuki hao wa Tabora wanarudi kwenye Uwanja wa nyumbani baada ya kuwa nje kwa takribani siku 11 ambapo mchezo wa mwisho kuchezwa kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi ilikuwa ni dhidi ya Geita uliomalizika kwa sare pacha kabla ya kusafiri kuelekea Jijini Dar es Salaam.

Tabora United chini ya kocha Mkuu Masoud Juma Irambona  imefanya maandalizi yake ya mwisho mapema leo na kwamba wachezaji wote wapo tayari kwa ajili ya kuzisaka alama tatu muhimu.

“Tumerudi salama jana kutoka Mkoani Morogoro tulipomalizia ratiba yetu ya michezo mitatu ya ugenini tuliyokuwa nayo,  kwa maana tulianza Dar es Salaam mchezo wa kwanza michuano ya Kombe la CRDB Bank Federation hatua ya robo fainali dhidi ya Yanga ambapo tulitolewa ,  mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Simba ambao tulipoteza kwa magoli mawili kwa bila .

Ratiba yetu nyingine ilikuwa ni dhidi ya Mtibwa Sugar  pale Manungu Turiani mkoani Morogoro,  pia tulipoteza kwa magoli matutu kwa bila, sasa tumerudi nyumbani kupambania nafai yetu ya kuendelea kusalia kucheza Ligi Kuu ya NBC Soka Tanzania Bara.

Tunafahamu kabisa kuwa hautakuwa mchezo mwepesi kwa sababu kila Timu inahitaji kufanya vizuri kwa maana ya kuvuna alama zote tatu ili kuweza kujiimarisha kwenye msimamo, tumejiandaa kupambana na tunaamini kuwa kila kitu kitakuwa sawa”.

Kwa upande wa Afya za wachezaji wote wapo vizuri, wanahari, morali na kwamba kila mmoja yupo tayari kutumika kesho isipokuwa,  tutawakosa wachezaji wawili kutokana na changamoto mbalimbali, Jerome Lambele amefiwa na dada yake hivyo amekwenda kwenye msiba nyumbani kwao Kigoma , Emotan Cletus bado anasumbuliwa na nyama za paja. 

Related Posts