Dodoma. Watuhumiwa wawili wanaokabiliwa na kesi ya mauaji ya mtoto wa Grayson Kanyenye (6) wamefikishwa mahakamani jijini Dodoma leo Jumatatu, Desemba 30,2024.
Mpaka sasa bado haijajulikana kesi hiyo itasomwa katika mahakama gani.
Grayson, mtoto wa mfanyabiashara maarufu jijini hapa, Zainab Zengo maarufu ‘Jojo’ anadaiwa kuuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani wakati mama yake akiwa matembezini usiku wa kuamkia Desemba 25, 2024.
Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi