RAIS SAMIA ACHANGIA MILIONI 35 UJENZI WA KANISA ANGLICAN MAKAMBAKO

News Njombe

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan amechangia Shilingili Milioni 35 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa kanisa la Anglikana Tanzania dayosisi ya Western Tanganyika lililopo katika Jimbo la Makambako mkoani Njombe.

Akikabidhi mchango huo kwa niaba ya Rais wakati wa harambee iliyofanyika kanisani hapo katika kata ya Maguvani,mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka amesema Rais anatambua mchango wa makanisa katika kudumisha amani nchini huku akiwataka wananchi kuendelea kuunga mkono Juhudi za Rais kwa kufanya kazi ili kukuza uchumi wao.

“Kupitia maombi yenu baba Askofu aliandika barua kwa Mh Rais na kwa uzito wa baba Askofu amejibu ile barua,kwa niaba yake ninawasilisha sadaka hii ya Mh Rais shilingi Milioni thelathini na tano na huu ni upendo mkubwa sana wa Rais kwa watu wa Njombe “amesema Mtaka

Askofu wa Kanisa Anglican Mathew Mhagama ameshukuru kwa Sadaka hiyo huku wakiahidi kutumia kwa uaminifu kulingana na maombi ya kanisa.”Fedha hizi tutazitumia kwa uaminifu kadri ya kile ambacho tumemuomba na utupelekee shukrani zetu”

Jumla ya Shilingi Milioni 60,123,000/= kati ya Milioni 310,000,000/= zinazohitajika kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa kanisa pamoja na ununuzi wa gari zimepatikana katika harambee hiyo iliyowakutanisha waumini na wadau mbalimbali akiwemo Mbunge wa jimbo la Makambako Deo Sanga pamoja na mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo.

 

Related Posts