Mwanasheria Mkuu mstaafu Jaji Werema afariki dunia

Dar es Salaam. Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) mstaafu, Jaji Frederick Werema (69), amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akipokuwa akipatiwa matibabu.

Taarifa ya kifo chake imethibitishwa na Katibu wa Halmashauri ya Walei, Parokia ya Mtakatibu Martha Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Salome Ntaro.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Jaji Werema amefariki dunia mchana wa leo, Jumatatu Desemba 30, 2024 katika hospitali hiyo, huku taratibu nyingine zikiendelea kupangwa na umma utajulishwa.

“Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa ya kifo cha mwenyekiti wetu wa Parokia ya Martha Jaji na Mwanasheria Mkuu mstaafu, mzee wetu Frederick Werema, kilichotokea mchana wa leo katika Hospitali ya Muhimbili,” ameeleza Salome katika taarifa hiyo.

Mbali na ubobezi katika taaluma ya sheria unaojulikana na wengi, Jaji Werema amewahi kuwa Mwalimu wa Shule ya Sekondari Shaaban Robert, jijini Dar es Salaam kati ya mwaka 1979 hadi 1980.

Sambamba na nafasi hiyo, pia amekuwa wakili tangu mwaka 1984 hadi 2006 na baadaye 2009 aliteuliwa kuwa AG, nafasi aliyohudumu hadi mwaka 2014 alipojiuzulu.

Pia, amewahi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu katika Divisheni ya Biashara

Related Posts