Jaji Werema kuzikwa Januari 4 Butiama

Dar es Salaam. Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema anatarajiwa kuzikwa Jumamosi Januari 4, 2025 Butiama mkoani Mara.

Ratiba rasmi ya mazishi iliyotolewa na familia yake ambayo Mwananchi imeiona imeeleza kuwa, Januari 1, 2025 ibada ya kumuombea marehemu itafanyika katika Kanisa la Mtakatifu Martha, Mikocheni jijini Dar es Salaam kuanzia saa 9 alasiri.

Aidha, Alhamisi Januari 2, 2024 shughuli za mazishi ya kiserikali zinatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaa kisha Januari 3, 2024 mwili wake utaondoka Uwanja wa ndege kuelekea Butiama.

Jaji Werema alifariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akipokuwa akipatiwa matibabu Jumatatu Desemba 30, 2024.

Kwa sasa msiba upo nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi

Related Posts