Njombe. Mahakama Kuu Kanda ya Iringa imewaachia huru makada watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliokuwa wameshitakiwa kwa tuhuma za mauaji ya kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Makada walioachiliwa huru ni George Sanga, Gudluck Mfuse na Octatus Mkwela, ambao kwa pamoja walikuwa wakituhumiwa kwa mauaji ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) kwa vyuo vikuu Mkoa wa Iringa, Emmanuel Mlelwa.
Katika kesi Na.52 ya mwaka 2024, washitakiwa hao walikuwa wakitumiwa kutenda kosa hilo walilodaiwa kulifanya mwaka 2020.
Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi