Planet, Eagles ngoma mbichi Mwanza

TIMU ya kikapu ya Eagles imeifunga Planet kwa pointi 63-55 katika fainali ya tatu ya Ligi ya Kikapu Mkoa wa Mwanza (MRBA) iliyofanyika katika Uwanja wa Mirongo mjini humo.

Kwa matokeo hayo Planet inaongoza kwa kushinda michezo 2-1.

Katika fainali ya nne endapo Eagles itashinda tena  matokeo yatakuwa 2-2 na mchezo wa tano utachezwa

huku timu itakayoshinda katika fainali hiyo itakuwa  bingwa kwa ushindi wa michezo 3-2.

Fainali hiyo ya kikapu inachezwa kwa timu kucheza michezo mitano (best of five play off), ambapo katika mchezo wa kwanza Planet ilishinda kwa pointi 71-53, huku ule wa pili ikishinda 67-62, ilhali Eagles ikishinda katika fainali ya tatu kwa pointi 63-55.

Katika fainali ya tatu, Eagles iliongoza kwa pointi 24-11, 16-23, 7-12 na 16-9.

Related Posts