Davidson anatupia huyo! | Mwanaspoti

NYOTA wa Christ the King, Davidson Evarist anaongoza kwa kufunga pointi 300 katika Ligi ya Kikapu Daraja la Kwanza inayoendelea jijini Dar es Salaam.

Nafasi ya pili kwa ufungaji inashikwa na Fahmi Hamad wa aliyefunga pointi 232, huku wengine wanaofuatia na alama walizofunga ni Diocres Mugoba (Premier 227), George Mwakyanjala (Yellow Jacket 186), Ally Songoro (Magone 175) na Dickson Thomas (Kigamboni 175).

Wengine ni Martine Rodgers (Mlimani B.C 173), Jackson Mrisho (Mbezi Beach 173), Lawi Mwambasi (Polisi 168) na Jacobu Malenga wa Chang’ombe aliyefunga 167.

Kwa upande wa udakaji wa mipira ya rebound  aliyeongoza ni Wilson Petar aliyedaka mara 133 sawa na Lawi Mwambasi wa Polisi aliyedaka pia mara 133.

Wachezaji wengine ni Hillary Ferix (Kurasini Heat)  na Abuu Hassan (Kibada Heroes) kila mmoja mara 100, Lawrence James (Dar King 98) na Fahmi Hamad (Polisi 95).

Wengine ni Emanuel Mwikalo (Yellow Jacket 91), Baraka Kweka (Mlimani B.C 86), Denis Jomalema (Magnet 84) na Francis Mallya wa Mgulani Warriors 82.

Related Posts