Kurasini Heat inavyozichanga kurudi BDL

POINTI 27-11 zilizofungwa na Kurasini Heat katika robo ya nne zilichangia kuishinda Premier Academy  kwa 70-61 katika mchezo Ligi ya Kikapu Daraja la Kwanza Mkoa wa Dar es Salaam uliopigwa kwenye viwanja vya Kurasini.

Kabla ya hapo, Premier Academy ilikuwa inaongoza kwa pointi 50-43.

Katika mchezo huo Premier Academy iliongoza katika robo ya kwanza kwa pointi 19-9, 18-18 na hadi kufikia mapumziko ilikuwa inaongoza kwa pointi 37-27.

Kurasini Heat iliyokuwa bingwa wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL) mwaka 2020 iliongoza robo ya tatu kwa pointi 16-13 na ya nne ikashinda 27-11, ikiwa imepania kurejea katika mashindano makubwa ya mkoa huko.

Katika mchezo huo, Hillary Felix wa Kurasini Heat alifunga alama 19 akifuatiwa na Anset Maliselo na Dominic Zacharia waliofunga 16 na 15 mtawalia.

Kwa upande wa Premier alikuwa ni Diocres Mugoba aliyefunga pointi 20 akifuatiwa na Calvin Mushi pointi 17.

Nahodha wa timu ya Kurasini Heat, Dominiki Zacharia  alisema ushindi wao umewanyoshea njia ya kucheza hatua ya robo fainali ya mashindano hayo.

Hata hivyo alikiri mchezo huo likuwa mgumu kutokana na ushindani waliokutana nao.

“Kwa kweli uzoefu wetu ndiyo uliochangia kushinda mchezo huo,” alisema Zacharia

Stephen Ollo, kocha wa Premier Academy, alisema kukosekana kwa wachezaji wake nyota wanne kulichangia  kupoteza mchezo huo.

Aliwataja wachezaji hao kuwa ni Franco Frank, John Magembe, Frank Maselo na Elisante Mpukwini.

Related Posts