DC Mgomi akumbusha jamii kujitoa kwa ajili ya wengine

Na Mwandishi Wetu

Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mheshimiwa Farida Mgomi amewaasa wananchi kuwa na utamaduni wa kuwashika mkono na kutoa misaada kwa makundi yenye uhitaji maalumu katika jamii, kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wameigusa jamii na kuipa Faraja katika nyakati zote.

Akizungumza wakati wa hafla ya kutoa misaada katika kituo cha Watoto yatima cha Hospitali ya Isoko kilichopo Kata ya Kafule wilayani hapa, ambayo imeongozwa na kikundi cha Wandali waishio Tunduma, Dc Mgomi amesema kuigusa jamii yenye uhitaji maalumu ni kitendo cha kujipatia baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu hivyo jamii inatakiwa kufanya hivyo.

Naye Mbunge wa Viti maalumu Mhe Stella Fiyao ambaye aliambatana na kikundi cha Wandali katika hafla hiyo, ameahidi kuwa kikundi hicho kitaendelea kuigusa na kuipa Faraja jamii kupitia misaada mbalimbali watakayokuwa wakiitoa na litakuwa zoezi endelevu la kuigusa jamii.

Misaada uliyokabidhiwa siku ya leo na pamoja na vyakula pamoja na mahitaji mbalimbali kama Mafuta, Taulo Za Kike, Mashuka, Sabuni Za Kuogea Na Kufulia, Sukari, Chumvi, Nguo, Madaftari na Kalamu ambapo kwa ujumla msaada huo umegharimu takiribani shilingi million Tatu.
Mkuu wa Wilaya ya Ileje Farida Mgomi akizungumza wakati wa hafla ya kutoa misaada katika kituo cha Watoto yatima cha Hospitali ya Isoko kilichopo Kata ya Kafule
 

Mkuu wa Wilaya ya Ileje Farida Mgomi akizungumza akitoa msaada wa daftari wa kituo cha Watoto yatima cha Hospitali ya Isoko kilichopo Kata ya Kafule.
 

Mkuu wa Wilaya ya Ileje Farida Mgomi akiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhi msaada vitu mbalimbali  kwenye  kituo cha Watoto yatima cha Hospitali ya Isoko kilichopo Kata ya Kafule


 

Matukio katika picha ya Mkuu wa Wilaya ya Ileje  Farida Mgomi katika kituo cha Watoto yatima cha Hospitali ya Isoko kilichopo Kata ya Kafule

Related Posts