RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AREJESHA TABASAMU KWA WANAFUNZI WENYE ULEMAVU MOSHI

NA WILLIUM PAUL, MOSHI.

NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera Bunge na Uratibu, Ummy Nderiananga amekabidhi viti mwendo na vifaa vya shule kwa watoto wenye ulemavu ili kuwarahisishia kufika shule.

Naibu Waziri huyo alikabidhi viti hivo kumi ambapo shughuli hiyo ilifanyika katika ukumbu wa halmashauri ya Moshi (KDC) wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo alisema kuwa lengo la Rais Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha watoto wote wanapata elimu bora.

“Katika kuhakikisha watoto wenye ulemavu na ninyi mnasoma kwa furaha Rais ameleta viti mwendo hivi ambapo mtavitumia kufika shule lakini pia tunawapa madaftari, mabegi na kalamu ili shule zinapofunguliwa na ninyi muwe tayari kwa kuanza masomo” Alisema Naibu Waziri Ummy.

Ummy alisema kuwa, halmashauri ya Moshi imekuwa ikitoa msisitizo mkubwa kwa watu wenye ulemavu ikiwa ni juhudi za kumuunga mkono Rais Samia katika kuwahudumia watu wenye ulemavu na kuzitaka halmashauri nyingine Kwenda kujifunza jinsi ya kwalea watu hao katika halmashauri hiyo.

Naibu Waziri huyo aliwataka wazazi na walezi wenye ulemavu kutambua kuwa Watoto hao wanauwezo mkubwa na kuwataka kukokata tamaa kwani wanaweza kufikia ndoto walizokuwa nazo.

“Rais amefanya juhudi kubwa kwa watu wenye ulemavu mkiona vifaa hivi tunaleta nay eye ameweka fedha kwa ajili ya kupata vifaa vya wanafunzi vya kujifunza na kufundishia kuanzia shule ya msingi mpaka vyuo vikuu” alisema Naibu Waziri Ummy.

Na kuongeza “ mwezi uliopita nilikuwa nagawa vifaa kama mfano kwa vyuo vikuu Rais ameweka fedha kwa ajili ya kununua vifaa vya kujifunzia wanafunzi wenye ulemavu wa vyuo vikuu kupitia wizara ya Elimu ambapo mwanafunzi anataja hitaji lake ni kitu gani anataka ili asome vizuri kwa hiyo vyuo vikuu 19 vikiwemo vyuo vya Zanzibar vimepata fursa hiyo”.

Alitumia nafasi hiyo kuitaka jamii kutowaficha ndani Watoto wenye ulemavu kwani serikali imeendelea kuboresha sekta ya elimu na sekta nyingine kuhakikisha kuwa Watoto wenye ulemavu nao wananufaika na miradi hiyo.

Awali akisoma taarifa kwa Naibu Waziri, Afisa Elimu Maalum Msingi katika halmashauri hiyo, Innocent Kahoko alisema kuwa, wanakabiliwa uhaba na uchakavu wa miundo mbinu ya majengo kwenye vitengo vya wanafunzi wenye ulemavu wa akili.

Alisema kuwa, wapo baadhi ya watumishi watatu wenye ulemavu ambapo wanauhitaji wa vifaa maalum vya kufanyia kazi ili kuweza kuwarahishia kufanya kazi zao kwa weledi mkubwa.




Related Posts