Bondia aliyefariki ulingoni azikwa Dar

Mazishi ya aliyekuwa bondia wa ngumi za kulipwa nchini Tanzania, marehemu Hassan Mgaya, yamefanyika leo Alhamisi Januari 2, 2025 kwenye makaburi ya Jeti Lumo jijini Dar es Salaam.

Mgaya alifariki Desemba 29, 2024 katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam kufuatia kupigwa kwa TKO na mpinzani wake Paulo Elias katika pambano lililofanyika usiku wa Desemba 27, 2024 kwenye ukumbi wa Dunia Ndogo uliopo Tandale kwa Mtogole.

Awali mazishi ya Mgaya yalipangwa kufanyika jana Jumatano Januari 1, 2025 lakini yaliyosegwa mbele hadi leo Januari 2, 2025 ili kutoa fursa kwa baba yake mzazi aliyekuwa nchini DR Congo kwenye majukumu ya kazi kushiriki.

Chama cha Mabondia wa Kulipwa Tanzania (TPBA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) sambamba na wadau wengine wa mchezo wa ngumi wameshiriki kikamilifu katika mazishi hayo kuanzia mwanzo hadi mwisho.
 

Related Posts