Maxi, Chama na Yao kuikosa TP Mazembe kesho

Mastaa watatu wa Yanga, Maxi Nzengeli, Clatous Chama, Yao Kouassi ni miongoni mwa wachezaji wanne ambao wataukosa mchezo wa kesho wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya TP Mazembe kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam mwingine akiwa ni Aziz Andabwile.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Yanga, imeeleza kuwa Chama anaendelea na matibabu ya jeraha la mkono huku Yao akiendelea na matibabu ya jeraha la goti.

Maxi na Andambwile wameshaanza mazoezi lakini hawajawa tayari kwa mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa kesho kuanzia saa 10:00 jioni.

Yanga kwa sasa inaburuza mkia katika msimamo wa kundi A ikiwa na pointi moja baada ya kucheza mechi tatu, ikipoteza miwili na kutoa sare moja.

Msimamo wa kundi A
1.Al Hilal- 9
2. MC Alger- 4
3. TP Mazembe – 2
4. Yanga – 1.

Related Posts