Jaji Merchan amesema Trump, rais wa kwanza wa zamani kuwahi kuhukumiwa kwa uhalifu, anaweza kujitokeza ana kwa ana au kwa njia ya mtandao katika hukumu iliyopangwa kusomwa Januari 10.Watoa uamuzi wa mahakama kuanza kujadili kesi ya Trump
Katika uamuzi wa kurasa 18, Merchan alikataa hoja mbalimbali za mawakili wa Trump wakitaka hukumu yake kutupiliwa mbali.
Jaji huyo amebainisha kwamba hana nia ya kutoa adhabu ya kifungo jela, badala yake anaegemea katika kuachiliwa bila masharti, hukumu nyepesi ambayo hata hivyo itamfanya Trump aingie Ikulu ya White House kama mhalifu aliyepatikana na hatia. Trump anatarajiwa kukata rufaa ambayo inaweza kuchelewesha hukumu yake.
Trump alipatikana na hatia huko New Yorkmnamo mwezi Mei kwa makosa 34 ya kughushi rekodi za biashara ili kuficha malipo ya pesa kwa nyota wa filamu za ngono Stormy Daniels kabla ya uchaguzi wa 2016.
Mawakili wake walikuwa wakitaka kesi hiyo itupiliwe mbali kwa misingi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na uamuzi wa kihistoria wa Mahakama ya Juu mwaka jana kwamba marais wa zamani wa Marekani wana kinga ya kutoshtakiwa kutokana na vitendo mbalimbali vya kiofisi vilivyofanywa wakiwa madarakani.Trump apatikana na hatia katika kesi ya uhalifu
Hata hivyo Jaji Merchan alikataa hoja hiyo lakini alibainisha kuwa Trump hataweza kushtakiwa mara tu atakapoapishwa kama rais.
Msemaji wa Trump, Steven Cheung ameshutumu uamuzi wa Jaji Merchan wa kutoa hukumu kwa rais huyo wa zamani, akiuita “ukiukaji wa moja kwa moja wa uamuzi wa kinga ya Mahakama ya Juu na sheria zingine za muda mrefu.”Kesi ya kihistoria dhidi ya Trump yaanza New York
“Kesi hii ya uvunjaji sheria haikupaswa kamwe kuletwa na Katiba inataka itupiliwe mbali mara moja,” alisema Cheung katika taarifa yake.
Cheung ameongeza kuwa hakupaswi kuwepo na hukumu, na Rais Trump ataendelea kupigana dhidi ya udanganyifu huo hadi utakapokoma.
Soma: Ipi hatma ya kesi zinazomkabili Donald Trump?
Trump pia alikabiliwa na kesi mbili za shirikisho zilizoletwa na wakili maalum Jack Smith lakini zote mbili zilitupiliwa mbali chini ya sera ya muda mrefu ya kutomshtaki rais aliyekuwa mamlakani.
Katika kesi hizo, Trump alishutumiwa kwa kula njama ya kutengua matokeo ya uchaguzi wa 2020 aliyoshindwa na Joe Biden na kuondoa idadi kubwa ya nyaraka za siri baada ya kuondoka Ikulu ya Marekani.